GET /api/v0.1/hansard/entries/205478/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 205478,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/205478/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kingi",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker": {
        "id": 248,
        "legal_name": "Joseph Kahindi Kingi",
        "slug": "joseph-kingi"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuzungumza machache kuhusu Hoja hii. Kwanza ninataka kumpongeza Waziri na Wizara yake; maafisa wake wote, kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kufanya katika Wizara hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaungana na wenzangu walionitangulia katika kutoa pongezi zao, hasa ukiangalia kazi nzuri inayofanywa na mashirika mbalimbali chini ya Wizara hii. Kuna Shirika la Kenya Airways ambalo linafanya kazi nzuri. Ninaamini kwamba kazi hii nzuri inaendelea kwa sababu ya usimamizi bora. Kuna mashirika mengine pia kama lile la Kenya Ports Authority (KPA), ambalo pia linafanya vizuri. Ninafikiri linafanya vizuri kwa sababu ya usimamizi bora. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninataka kumpogeza Waziri na kumuuliza aendelee kufanya kazi hio nzuri. Sehemu hizi ambazo tunazitaja zinazohitaji marekebisho zifanyiwe marekebisho ili 3722 PARLIAMENTARY DEBATES September 5, 2007 kazi yao izidi kuwa nzuri. Bw. Naibu Spika wa Muda, wenzangu waheshimiwa wamezungumuzia ajali barabarani. Tumepoteza watu wengi. Hivi majuzi kulikuwa na ajali mbili mbaya sana. Hili si jambo ambalo tunalotaka kuliona. Sitarudia sababu walizotaja kusababisha ajali za barabarani. Lakini ninataka nitaje kwamba kuna wakati nilishuhudua ajali. Tulipokuwa tunataka kuwasaidia wale waliojeruhiwa, kuna jambo moja ambalo tuligundua. Wengi wa wenye magari hupuuza sheria zingine kama vile kubeba visanduku vya huduma ya kwanza na vifaa vya kuzima moto. Hivi vifaa ni muhimu sana. Ingawaje sheria inaeleza kwamba viweko katika magari ya usafiri, mengi huwa hapana. Wale wakonavyo, utakuta kwamba viko duni. Labda sababu moja ni kwamba Wizara haijaelezea vifaa hivi viwe vya namna gani. Ikiwa ni kisanduku cha huduma ya kwanza, ni vifaa gani vinahitajika kupatikana ndani ya kisanduku hicho. Ikiwa ni vifaa vya kuzima moto, basi vitakuwa namna gani. Hata polisi wanaposimamisha magari kufanya ukaguzi, wahakikishe vifaa vile vinavyohitajika vipo ndani ya magari. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninataka nizungumuzie feri. Watu wengi wa Pwani wanaishi kusini mwa Pwani au South Coast . Kuna shughuli nyingi za ukulima, utalii na za uchimbaji wa madini ya titanium. Bila shaka, kutakuwa na kazi nyingi. Watu wengi wanaoishi Pwani Kusini, South Coast; huenda pia Pwani Kaskazini, North Coast, na vifaa wanavyotumia kuvuka ni ferry . Lakini nashangaa kuona kwamba nyingi ya zile ferry zinazotumika kufikia sasa zimezeeka; ni za kitambo sana; zina umri wa zaidi ya miaka 30. Mara nyingi ferry hizi zimekwama katikati ya Bahari kwa sababu hazina nguvu na uwezo wa kuwavukisha wananchi. Bw. Naibu Spika wa Muda, miaka michache iliyopita tulikuwa na ajali mbaya sana ya ferry huko Mtongwe ambapo Wakenya wengi walipoteza maisha yao. Mpaka sasa nafikiri Wizara bado inaendelea kulipa ridhaa kwa familia ambazo zilipatwa na mkasa huo. Hatutaki kuona ajali kama hiyo ikitokea tena. Tumekuwa tukifuatilia mambo haya ya ferry . Tunajua kwamba kibali kilipeanwa kwa Kenya Ferry Services (KFS) inunue ferry mpya, na hatujui ni matatizo gani yamewazuia kuinunua, ili kuhakikisha kwamba maisha ya Wakenya yatakuwa salama. Hatutaki kuona mkasa mwingine kama huo uliotokea miaka michache iliyopita ukitokea tena Likoni. Ferry hizi huwa zinabeba watu wengi sana. Nafikiri kuna nyingine ambazo hubeba watu zaidi ya 1,000, na haitakuwa vizuri sisi tukae ilhali ferry zetu ziko katika hali hiyo. Wenzangu wamezungumzia kuhusu reli. Reli ni muhimu na tungetaka kuona Wizara hii ikisambaza huduma za reli kila mahali katika taifa hili. Tangu tukiwa watoto wadogo tuliona laini moja tu ya reli kutoka Mombasa kupitia Nairobi hadi Kisumu, na kengine kafupi kutoka Voi kwenda sehemu za Taveta. Hakujafanywa juhudi zozote za kusambaza huduma za reli katika taifa hili. Tunataka huduma za reli zisambazwe kila mahali, kwa sababu kila mahali wananchi wanafanya kazi, wanalima na wangetaka kusafirisha bidhaa zao bila matatizo. Tungetaka pia huduma za reli ziimarishwe kati ya Mombasa na Nairobi ili mizigo mizito mizito inayopokelewa leo iondolewe kutoka barabarani na kusafirishwa kwa reli ili tuweze kulinda barabara tunazojenga. Ujenzi wa barabara ni ghali na tunatumia pesa nyingi. Lakini iwapo magari mazito mazito, ambayo mengine yana zaidi ya tani 50, hatutayaondoa kutoka barabara zetu, basi tutakukuwa tukijenga barabara kila mwaka, na kwa hivyo hatutaweza kuendelea. Tungetaka reli ijengwe hadi Lamu, Malindi, Ganze, Kinango na Kwale ili tuweze kuwasaidia wakulima, wavuvi na watu wengine ambao wangetaka kupeleka bidhaa zao katika Mji wa Mombasa. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunapozungumzia viwanja vya ndege, nataka kuongeza tu kwamba kwa miaka mingi tumesikia hadithi kuhusu upanuzi wa uwanja wa ndege wa Malindi. Tungetaka kuona ndoto hii ikiafikiwa. Wakaazi wa Malindi, na Mkoa wa Pwani kwa jumla, wangetaka kuona viwanja vya ndege vya Malindi, Diani, Isiolo na hata katika sehemu nyingine kama vile Mandera vikidumishwa ili wasafiri wetu waweze kusafiri kwa usalama. Kunazo sehemu nyingine ambako viwanja vyake vya ndege nafikiri vilinyakuliwa na mabepari. Moja ya sehemu September 5, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3723 hizo ninayoijua wazi ni Kilifi. Kile kiwanja cha ndege cha Kilifi kilinyakuliwa na sasa Kilifi ina shida, haina uwanja wa ndege. Tungetaka kuuliza Wizara ichukue hatua inayohitajika ili watu wa Kilifi wapate uwanja wao. Pia infaa Wizara iutengeneze vizuri huo uwanja ili wakaazi wa Kilifi nao waweze kupata huduma ya kiwanja hicho. Ningetaka pia kuongeza kwamba ni vizuri madereva wetu, hasa wanaoendesha gari za abiria, iwe mara kwa mara wanafanyiwa ukaguzi. Ingekuwa vizuri pia tubadilishe mfumo wa kutoa leseni. Labda tungezitengeneza upya na kuzifanya kuwa electronic ili maafisa wa polisi wanaofanya ukaguzi mara kwa mara waweze kuweka alama katika leseni, hasa katika zile za madereva wanaofanya makosa. Sasa hivi hili jambo halifanyiki kwa sababu tunatumia leseni za zamani sana, na inakuwa vigumu kujua madereva wanaofanya makosa mara kwa mara. Hili ni jambo ambalo linafanywa na jirani zetu---"
}