HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 205648,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/205648/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii, ambayo ni muhimu sana. Namaanisha Hoja ya Wizara ya Uchukuzi. Kwa kweli, kulingana na umuhimu wa hii Hoja, watu wengi sana wangehusika. Mawaziri wa Serikali hii wangekuwa hapa kwa wingi ili kusikiliza Hoja hii kwa sababu inahusu sehemu zote. Nafikiri, labda, watu wamechoka. Serikali hii imechoka! Basi, livunje Bunge hili mara moja ili watu waende nyumbani kwa uchaguzi mwingine mpya! Hatuwezi kuwa na Hoja muhimu kama hii na Serikali haionekani! Watu hao ndio wenye jukumu la kutupatia mwelekeo! Bunge hili lingevunjwa leo ama kesho, ili twende kwa uchaguzi mpya ili tuangalie sera mpya! Baada ya kusema hayo, Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kusema kwamba nimewasikiliza wale wenzangu waliochangia kwa kirefu. Michango yote imekuwa muhimu kwa sababu imesisitiza umuhimu hasa wa Wizara hii kuwa na maono. Jukumu kubwa ni kuwa na 3710 PARLIAMENTARY DEBATES September 5, 2007 ndoto. Jambo muhimu ambalo lingefanywa na Wizara ya Uchukuzi ni kukabiliana na suala la usafiri katika karne hii. Inajulikana wazi kabisa kwamba tunalia kuwa barabara zimeharibika kwa sababu ya malori makubwa yanayobeba mizigo kupitia nchi yetu na kuipeleka huko Congo, Sudan, Rwanda na Burundi. Lakini, tatizo ni kwamba binadamu wamegundua kwamba usafiri wa reli ndio msingi hasa wa usafirishaji nchini. Kwa hivyo, badala ya Wizara ya Uchukuzi na Serikali kuzungumzia mambo ya ubinafsishaji wa mambo muhimu kama reli--- Umekuwa kama wimbo! Serikali ingechukua sekta ya usafirishaji na kuifanya imara zaidi. Sekta hiyo ndiyo msingi wa uchumi wa nchi hii! Tunafikiria kwamba badala ya Serikali kuichukua reli na kuipatia watu wa Afrika Kusini, ingehusika zaidi! Tangu tuwe huru mpaka sasa, tunawakubali wawekezaji wa kila aina. Kwa mfano, kuna wawekezaji wa kuuza bia, nyama choma, kuku na mayai. Yaani, tunawakaribisha watu kufanya mambo mengi katika mahoteli. Wizara hii ingetembea dunia nzima kutafuta wawekezaji wa reli na kufanya kazi pamoja nao. Hilo ndilo jukumu kubwa zaidi, badala ya kuwakaribisha watu kuja kufanya mambo ambayo Wakenya wenyewe wanaweza kuyafanya. Isitoshe, mambo hayo yanahitaji ujasiri! Zamani, wakati reli hii ya Uganda ilipojengwa, ilichukua miaka mitano. Wazungu wakoloni na watu wengine walikaa porini na kujenga reli kwa mikono. Makalasinga waliletwa kutoka nje chini ya serikali ya mkoloni, watu walipanda na kupitia kwenye mbuga ambazo hazijulikani! Walitumia teknolojia ya chini na wakajenga reli kutoka Mombasa hadi huko Port Florence au Kisumu ya sasa! Mpaka sasa, sisi Waafrika katika dunia ya leo, ujasiri wetu uko wapi? Naamini kwamba kukiwa na ujasiri wa kuwahamasisha wananchi wa Kenya na dola kuipa reli kipa umbele, hilo ni jambo ambalo linaweza kutokea. Lakini tukiwa na mawazo kuwa tutakuja kufanyiwa mambo na mabepari au watu binafsi ambao watawekeza, na dola itolewe huko, sijui kama kuna pahali tuaenda. Isitoshe, reli inawaajiri kazi wananchi wengi sana. Kwa hivyo, namuomba Waziri wa Uchukuzi awaangalie wale watu waliokuwa wameajiriwa na Shirika la Reli la Kenya Kenya na Shirika la Reli la Afrika Mashariki na ahakikishe kwamba wamelipwa kikamilifu kutokana na jasho lao. Kuna malalamiko makubwa sana na watu wanateseka. Watu ambao walikuwa wanafanya kazi kwenye shirika la Reli hawajalipwa ajira yao. Tunadai kwamba lazima hiyo ajira ipatikane. Inatakikana tufikirie juu ya miundo msingi ambayo tumepata kibahati kama bandari. Serikali isijiondoe kwa bandari ila ifanye mipango ya kurekebisha yale matatizo na kufanya bandari iwe ya kisasa badala ya kuwa na fikra za kuibinafsisha. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaomba kwamba katika uajiri huko bandari, lazima tuhakikishe kwamba kuna haki ya kuajiri. Vibarua wamezidi huko Mombasa bandarini. Inafaa tuwe na juhudi ya kuajiri watu badala ya kuwafanya watu wengi kuwa vibarua kwa miaka mingi. Isitoshe, kusiwe na ubaguzi wa kikabila katika kuajiri watu. Inafaa tuhakikishe ya kwamba watu wanaajiriwa kwa haki. Ule msongomano wa magari kule Mariakani katika toll station na mahali pengine ni mbaya sana na hausaidii uchumi wetu. Watu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan, Burundi na Rwanda huwa wanachoka sana katika ule msongomano ambao unaletwa kwa kutokuwa na mpangilio mzuri katika hiyo toll station. Jambo lingine ambalo linazua malalamiko ni ufisadi. Kwa hivyo, lazima Serikali inyoroshe hayo pamoja na barabara kutoka bandari. Barabara ya kutoka Naivasha hadi Kisumu ni mbaya sana. Pia ile barabara ya kwenda Eldoret ni mbaya mno. Hiyo haiwezi kusaidia usafirishaji. Viwanja vidogo vidogo vya ndege ni muhimu sana kwa usalama, uchumi na utalii katika nchi. Ni muhimu viwanja vidogo virekebishwe. Kwa mfano, kiwanja cha Voi kimewachiliwa sana. Inafaa kitengenezwe. Kitasaidia sana kwa utalii kwa sababu kiko karibu na mpaka. Kitasaidia biashara mpakani na vile vile biashara ya madini. Vile vile, mji wa Voi unakua sana na kuna watu wengi. Kwa hivyo, kiwanja kama cha Voi kinastahili kurekebishwa ili ndege zianze kutua hapo. Bw. Naibu Spika wa Muda, lazima tukubali ya kwamba tunaagiza magari ya mitumba kupita kiasi. Tunalaumu watu kwa kunywa pombe ama kuendesha magari kwa kasi, lakini, labda September 5, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3711 mitumba ya magari ambayo imezidi katika hii nchi haiwezi kutuhakikishia usalama. Kwa hivyo, mikakati ifanywe ili hayo magari ya mitumba yaangaliwe kwa undani zaidi na hata yapunguzwe na ikiwezekana yaondolewe kabisa. Magari ni mengi kupita kiasi hapa Nairobi na kote nchini. Kuna misongamano mijini na ajali nyingi. Ni lazima tuhakikishe usalama wa wananchi wetu kwa kudhibiti uagizaji wa magari ya mitumba kutoka nje. Hiki pia ni chanzo kikubwa cha ajali ambazo zinatokea katika nchi yetu. Hata usafiri wa meli kwenye Ziwa Victoria ni muhimu uendelee. Sijaona uwekezaji wa Serikali katika biashara ya utalii katika miji ilioko karibu na Ziwa Victoria. Utalii utaweza kuendesha uchumi wetu katika hiyo miji mingi ambayo iko ndani ya Ziwa Victoria. Ni lazima Serikali iangalie hayo ili tuendeleze utalii katika Ziwa Victoria. Kwa ujumla, hii ni sekta ambayo ingepata pesa nyingi zaidi. Kwa hivyo, hii ni pesa kidogo sana. Tungeongeza pesa katika hii Wizara ya Usafirishaji lakini lazima iwe katika mstari wa mbele wa kutupatia sera na mwelekeo wa kusuluhisha tatizo la usafiri katika nchi yetu na kuifanya nchi yetu iwe ya kisasa. Ni lazima tuzingatie sekta ya reli na bandari ili ziimarishwe na kufanywa bora zaidi. Bw. Naibu Spika wa Muda, inafaa Serikali ionekane inahusika zaidi na sio kuwauzia watu binafsi. Kwa mfano, faida ikipatikana na Kenya Airways, inaenda kwa nani? Nyingi inaenda kwa watu binafsi. Watu binafsi wanatajirika zaidi. Hata ninashindwa hiyo ambayo tunaita Kenya Airways, ni kwa nini inabeba bendera ya Kenya na haiwafaidi Wakenya? Ningependa kuona ndege ya Kenya ambayo inabeba bendera ya Kenya, ikiwa ni mali ya dola ya Kenya, kwa niaba ya wananchi wa Kenya na sio mali ya mabepari binafsi ambao wanabeba bendera ya Kenya na kuzungusha huko na kusema kwamba wanafanya biashara kwa niaba ya watu binafsi. Mimi ninasisitiza kwamba lazima dola ihusike sana katika usafirishaji kwa sababu hiyo ndiyo inaonekana kote duniani. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}