GET /api/v0.1/hansard/entries/206406/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 206406,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206406/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nampongeza aliyewasilisha Hoja hii. Sehemu za nchi kame ama nusu-kame zina uwezo mkubwa sana. Kile ambacho hatuna ni mipango halisi na utekelezaji wa mipango hiyo. Katika Taita Taveta, kuna chemchemi za Mzima Springs. Ni maji ambayo yanatoka Mlima Kilimanjaro. Tuna madini mengi sana. Tuna mbuga za wanyama pori. Lakini bado Serikali haijatekeleza mipango hiyo. Maji yanatoka sehemu ya Taita Taveta na kumwagika baharini. Sehemu za nyando za chini za Taita Taveta ni nchi kame. Madini ambayo yanaweza kuleta mabilioni ya pesa yako kwa wingi. Lakini hayo mabilioni hayaingii kwa kodi ya wananchi. Yanaenda kutumika kiholela. Ardhi ya kufuga wanyama wa pori katika sehemu za nchi kavu ipo. Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Kinachohitajika ni utekelezaji na sio maneno matupu!"
}