GET /api/v0.1/hansard/entries/206541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 206541,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206541/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, wakati mwingine tunashindwa kuelewa ni nani hasa ambaye ana jukumu la kukarabati barabara hapa nchini. Kwa mfano, kuna barabara ya kutoka Wundanyi hadi Werugha. Barabara hii ilijengwa na kampuni ya Victory lakini imeharibika. Tunaambiwa kwamba itakarabatiwa, lakini hakuna jambo linaloendelea. Wakati huu watu wa Werugha wameulizwa na Mkuu wa Wilaya na chifu wakusanye mawe ili wairekebishe barabara hiyo. Je, ni nani hasa ambaye anahusika na ukarabati wa barabara ya Wundanyi kwenda Werugha?"
}