GET /api/v0.1/hansard/entries/206569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 206569,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206569/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": "Nimehama kwa sababu nimepigiwa kelele hapo mbele! Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa nasema kwamba kuna mabalozi ng'ambo ambao ningetaka kuwatolea pongezi zangu kwa sababu ya mapokezi na utumishi ambao wanatolea Wakenya wote ambao wanakutana nao. Hata hivyo, kuna mabalozi wengine ambao hawastahili pongezi kabisa. Inatakikana watie bidii katika kuboresha utumishi wanaotolea Wakenya. Mimi mwenyewe, kuna wakati nilikutana na jinamizi wakati mmoja nilipotembelea nchi ya Afrika Kusini. Nilifika huko saa sita za usiku, na hapakuwa na mtu yeyote kutoka kwa ubalozi wetu aliyekuja kunilaki. Ilikuwa niingie katika gari la wakora ili wanipeleke kule nilokokuwa nakwenda. Nilikuwa nimeenda huko kuhudhuria mkutano rasmi. Hata hivyo, niliokolewa na kijana mmoja Mkenya ambaye alinibeba katika gari lake. Tulizunguka kwa masaa matatu, kutoka saa sita hadi saa tisa usiku. Nilishangaa sana kwamba Waziri Msaidizi, kama mimi, anaweza kutembelea nchi fulani na balozi wetu asiwe na habari hiyo. Ninafikiri tuna aina mbili ya mabalozi. Kuna mabalozi wanasiasa na wale ambao wamepata kazi hiyo kwa sababu ya taaluma yao. Ni uzoefu wangu kwamba kila ninapotembelea nchi ambayo balozi wetu huko alikuwa mwanasiasa hapo awali, mimi hupata shida. Ukienda katika nchi ambayo balozi wetu huko ni mwanataaluma na amekuwa katika kazi hiyo kwa muda mrefu, utapata mapokezi tofauti. Wanasiasa wanapofeli katika uchaguzi na kuteuliwa kuwa mabalozi, wao August 29, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3571 huenda kule kujenga himaya zao! Katika hizo himaya, kuna wale wa kuhudumiwa na wale wasiostahili kuhudumiwa. Wakati nilipokuwa ninataabika kule, kulikuweko na balozi ambaye alikuwa amejaribu kuingia hapa Bungeni lakini akashindwa. Aliposhindwa alitupwa kule. Sijui ni kutupwa ama kuzawadiwa, sina habari. Lakini alipofika kule alijua kwamba amefika pahali ambapo anaweza kukalia hata wale ambao walifaulu pale ambapo alianguka. Bw. Naibu Spika wa Muda, hili ni jambo linalostahili kutazamwa upya. Kama tunataka kuwa na mabalozi watakaofanya kazi yao inavyotakikana basi wasiwe wanasiasa. Wanasiasa wafanye siasa na wanadiplomasia waachiwe kazi ya ubalozi. Haya mambo yasichanganywe! Kuchagua mtu kuwa balozi kwa sababu ni rafiki yako na amefeli ni makosa."
}