GET /api/v0.1/hansard/entries/206571/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 206571,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206571/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, sijali kama huyo mtu aliyechaguliwa alikuwa Rais au nini. Hawastahili! Wakae nyumbani ili wanadiplomasia wafanye kazi ya ubalozi. Tukifanya hivyo, utapata kwamba nidhamu na huduma zitaboreka sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, nitahitimisha kwa kusema kwamba ni makosa kuwachagua mabolozi kwa misingi ya vyama, ukabila na urafiki. Mtu wa aina hiyo, huwezi kujua uaminifu wake uko wapi. Ni vigumu kwake kuwa mwaminifu kwa Wakenya wote. Ndiyo sababu ninasema kwamba ni muhimu tutenganishe siasa na kazi ya ubalozi. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo ningetaka kuuliza, na labda Waziri atanieleozea: Ni kwa nini kuna maeneo mengine katika nchi hii ambayo hayajatoa balozi hata mmoja tangu Uhuru? Katika sehemu nyingine za nchi hii, utagundua kwamba panateuliwa mabalozi wawili, watatu hata watano! Kwa nini kuna ubaguzi huu? Ukienda kule kwetu Nakuru leo na uwaulize wananchi wakuambie ni watu wangapi kutoka Nakuru wameteuliwa kuwa mabalozi, watakuambia hakuna hata mmoja. Hata mmoja huwezi ukapata! Kama yupo, ningetaka niambiwe ni balozi fulani aliyeteuliwa kutoka Wilaya ya Nakuru. Hata hivyo, mimi sina habari. Kama vile hatuna wazaliwa wa Nakuru ambao wemekuwa wakuu wa wilaya. Kuna wakati tulikuwa na mkuu wa mkoa. Lakini hiyo ilikuwa ni bahati tu. Hatujapata katibu mkuu au"
}