GET /api/v0.1/hansard/entries/206581/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 206581,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206581/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna tatizo lingine ambalo ningependa tusaidiwe na Wizara ya Nchi za Kigeni. Hili jambo ni sifa mbaya ambayo Wakenya wamekuwa wakiipatia nchi hii. Ukisoma magazeti, utapata kwamba visa vya Wakenya wanaoshiriki katika kuharibu jina la nchi yetu huko ng'ambo vimeongezeka. Hivi majuzi tumesoma juu ya Wakenya waliofanya wizi huko Sudan. Aidha, juzi niliona katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Tanzania zaidi ya picha ishirini za Wakenya ambao wamehamia kule na wanafanya wizi. Isitoshe, tumekuwa tukisoma katika magazeti juu ya Wakenya wanaoshiriki katika wizi kule Marekani. Ninadhani kuna haja ya Wizara hii kutembelea Wakenya hawa na kuwafundisha kwamba hawakuenda ng'ambo kushiriki wizi. Wafanye kazi ambayo itakuwa faida kwao na kuiletea nchi yao sifa nzuri. Ikiwa Wakenya watapatikana tu katika shughuli za wizi, itakuwa ni bahati mbaya sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, nimewasahihisha mabalozi lakini ningetaka kusema kwamba kuna mabalozi ambao wanastahili kupewa sifa. Ningependa kuwataja baadhi yao: Balozi Amina; ambaye nilikutana naye Geneva, Balozi Kahindi, Balozi Kaikai na Balozi wetu kule New York. Mifano ambayo imetolewa na mabalozi hawa ni ya kuigwa na Wizara nzima. Kwa hayo, ninaomba kuunga mkono."
}