GET /api/v0.1/hansard/entries/206584/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 206584,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206584/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii nami nichangie kidogo kuhusu Hoja hii ya kuongezea pesa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni. Mwanzo, naomba kuunga mkono kwa sababu Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni inachangia sana kiuchumi. Biashara nyingi ambazo zinapatikana katika sehemu ya Uganda na Kanda ya Maziwa Makuu na sehemu zote ambazo ziko karibu na ng'ambo, nyuma yake kuna sera za Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni. Hilo linadhiirika wazi wakati unapotembea nje na kukutana na mabalozi ambao wanakusanya habari na kutupatia. Kwa hivyo, pamoja na hayo, naunga mkono sera ya kuhakisha kwamba ile mali tuko nayo nyumbani, tuendelee kuzihifadhi vizuri, ili ziwe zetu. Hapo, tutakuwa tumezihifadhi pesa katika nchi yetu badala ya kuendelea kuzilipa huko nje. Nasema hapa kwamba kuna haja ya kujenga ubalozi huko Abuja. Pia, ukiangalia huko Lagos, ile mission yetu ina ardhi kubwa na nzuri sana. Hata ikigawanywa mara mbili, inaweza kulipia ujenzi wa ubalozi mwingine huko Abuja na kuwacha consulate huko Lagos. Lakini baada ya kusema hivyo, tunajua kwamba maswala ya kidiplomasia yanahusu--- Sasa, kuna mambo yamezungumzwa hapa. Eti sasa, wakati wa \"vita baridi\" umeisha. Diplomasia sasa imekuwa ni maswala ya kiuchumi na kibiashara. Ingawa nakubaliana na hayo, tukumbuke ya kwamba diplomasia haihusu leo peke yake. Nchi hii ya Kenya itakuwa hapa hata miaka 1,000 ijayo. Kwa hivyo, lazima tuangalie maswala ya kidiplomasia kwa muda mrefu zaidi, kuliko maslahi ya sasa. Tukizingatia zaidi maswala ya leo, wakati fulani tutajikuta tunaibishwa aibishwa na kuharibu hata heshima ya nchi yetu, ili kupata maslahi ya leo tu. Tukumbuke kwamba tunapozungumza hapa--- Tukizungumzia swala la ugaidi, tunasikitika sana. Hasa sisi ambao tunatoka Mkoa wa Pwani, vijana wetu--- Federal Bureau of Investigations (FBI) na watu wa Central Intelligence Agency (CIA) wanaingia kwetu na kuwakamata watu wetu na kuwapeleka nje ya nchi yetu, na tunanyamaza! Eti ni diplomasia! Tuna maslahi kutoka Marekani! Watu wanakamatwa na kupelekwa hadi Ethiopia na Somalia, eti ni diplomasia. Jeshi la Uganda linaingia mpaka ndani ya mpaka wetu na kuchukua ng'ombe na kutatiza watu. Tunanyamaza eti ni diplomasia tunafuata. Tunafanya diplomasia mpaka tunakuwa na upungufu wa mambo ya ndani. Huko Somalia, Marekani inakuja na kuingia katika dakika ya mwisho na sisi tunanyamaza tu. Yale mambo ambayo tumeyapigania kwa muda mrefu na tumeyafanya maslahi yetu kwa muda mrefu--- Tumetoa hela nyingi. Tumesaidia watu wa Sudan kwa muda mrefu zaidi. Tumewasaidia watu wa Somalia kwa muda mrefu zaidi. Lakini dakika ya mwisho, Marekani inakuja na kuchukua kila kitu na kwenda. Tukiangalia, tunajiuliza: \"Sasa, maslahi yetu huko Democratic Republic of Congo (DRC) yako wapi?\" Biashara iko huko. Kila mtu anaenda huko! Nasikia hata Afrika Kusini inaenda huko. Sisi tunaheshimiwa zaidi kwa sababu wanatutambua. Tumetembea huko na wanaona sisi ni Waafrika. Tunazungumza lugha moja na tuna utamaduni unaowakaribia sana kuliko huko. Lakini sisi tunafanya nini kwa maslahi ya Burundi? Nasema tusiangalie maslahi ya hapa. Sisi tuna swala la Jumuia ya Afrika Mashariki. Nashukuru sana kwamba sasa, Jumuia ya Afrika Mashariki inahusu pia Rwanda na Burundi. Lakini tujue kwamba sisi Wakenya ndio tuna maslahi makubwa zaidi katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Kwa hivyo, tuendelee zaidi kusukuma na kutumia kila njia kujaribu kuhakikisha kwamba Jumuia ya Afrika Mashariki inafaulu. Wale wengine watasitasita kwa sababu hawaoni maslahi yetu. Sisi Wakenya tunajua tuko wapi. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba sisi ndio tunafanye kila kitu ili jumuia hiyo ifaulu. Bw. Naibu Spika wa Muda, mojawapo ya mambo huwa nasema ni kwamba, ili tuweze kuheshimika; na watu wanatuheshimu zaidi katika Afrika Mashariki, tujitayarishe kutoa"
}