GET /api/v0.1/hansard/entries/206586/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 206586,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206586/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "na tuwe na vyuo vingi zaidi. Tunaweza kuzipatia nchi zingine kama Burundi, Rwanda, Djibouti, Somalia na hata Sudan scholarships . Hata kama tuna matatizo yetu, tufanye kama Cuba. Wakati tunaendelea kujenga, tunaendelea kutoa. 3576 PARLIAMENTARY DEBATES August 29, 2007 Bw. Naibu Spika wa Muda, baada ya kusema hivyo, nashukuru kwamba watu wamesema tukichagua ubalozi, tusizingatie tu maslahi ya wanasiasa peke yake. Mimi nasikitika kusema kwamba mtu ambaye amestaafu kama Rais, na anapata pension kubwa mno - pesa nyingi kabisa - na ambaye hana matatizo, eti sasa amekuwa mwanadiplomasia wa amani huko Sudan. Tukiangalia rekodi yake ya kuunga mkono udikteta--- Na watu wengi wameteseka katika nchi hii! Rekodi hiyo ni mbaya sana katika nchi. Sasa hivi, watu wengi sana wameteseka. Watu wengi wamekufa. Vita vingi vimepiganwa ndani ya nchi hii. Halafu sasa, mtu huyo anaenda kuhubiri amani huko Sudan! Hiyo si diplomasia ya ukweli kabisa! Kama tunaweza kufanya hivyo, tunakosea kwa sababu lazima tupeleke mtu ambaye kwa kweli, akienda huko, atatoa picha ya amani. Labda tungempeleka Mt. Elgon! Anaweza kuzungumza lugha moja na kuwasaidia watu hapo karibu. Maanake ni mzee ambaye amestaafu na nyumbani kwake ni karibu na Mt. Elgon. Tuko na shida huko. Haidhuru, tungempeleka mzee kama huyo hapo. Lakini tukimpeleka huko Sudan, nafikiri tunakosea heshima ya nchi hii na udiplomasia. Bw. Naibu Spika wa Muda, tusifikirie ni wanasiasa peke yao. Kuna waandishi kama akina Ngugi wa Thiong'o ambao wanaheshimiwa kote duniani! Kuna Profesa Micere Mugo ambaye ni msomi na mwaandishi anayeheshimiwa. Kuna Prof. Ali Mazrui. Nashukuru kwamba yeye ni"
}