GET /api/v0.1/hansard/entries/206588/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 206588,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206588/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "wa Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT). Lakini hao ni mabalozi. Kuna akina Shadrack Guto. Hadi sasa, anatumiwa kama Balozi katika Afrika Kusini. Anaheshimiwa sana kwa mambo mengi ya kidiplomasia. Anatumwa hata na Rais Mbeki. Ukienda Namibia na kusini mwa Afrika, Wakenya wengi ndio wanafanya hivyo. Kuna Wakenya wengi ambao ni lazima tuwatambue na kuwapa nafasi kama hizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, mimi nafurahi sana na kuipongeza Wizara hii ya Mashauri ya Nchi za Kigeni kwa kufanya uhusiano, hasa na Cuba, kuwa mzuri. Hilo ni jambo nzuri sana kwa sababu nchi ya Cuba ina heshima sana kwa wale watu ambao wanapigania ubinadamu duniani. Na ile hofu ya kuumbishwa kidiplomasia na Marekani, ambayo imewazuia kwa muda mrefu--- Nashukuru kwamba Serikali imetumia huo msimamo. Naomba uzidishwe. Waende hata Venezuela na baadaye, hata tufungue ubalozi sehemu hizo. Kuna manufaa mengi sana ambayo tunaweza kuyapata kutoka Cuba na Venezuela. Nashukuru kwamba nchi kama hizo zinasaidia hata wanafunzi wetu ambao wanasoma huko. Nchi hizo ziko tayari kwa kutusaidia kwa mambo mbali mbali. Tunachoomba ni kwamba mikataba yote mizuri ambayo inatiwa sahihi na Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni na serikali zingine itekelezwe. Iwe inatekelezwa mara moja. Hapo, namaanisha ile ambayo ina manufaa kwa nchi yetu. Tusiwe tunatia sahihi mikataba halafu tunachelewa. Najua kuna mikataba mingi ambayo imetiwa sahihi kati ya Cuba na nchi yetu. Inangojea kutekelezwa. Tunataka mikataba hiyo itekelezwe, ili watu wetu wafaidi! Ile mikataba inayoletwa na Venezuela, tuifuate ili tupate maslahi ya haraka kwa ajili ya nchi yetu. Kwa maneno hayo machache, naomba kuunga mkono."
}