GET /api/v0.1/hansard/entries/206589/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 206589,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206589/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Awori",
"speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
"speaker": {
"id": 290,
"legal_name": "Moody Arthur Awori",
"slug": "moody-awori"
},
"content": " Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii na mimi, vile vile, niseme machache kuhusu Wizara hii. Wizara hii ni ya maana sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, wale walionena mbele yangu walikuwa wakiuliza: Ni sera gani iliyoko kuhusu balozi za Kenya? Kwa kweli, labda hakuna mjadala ambao umeandikwa chini ambao unaonyesha sera za balozi zetu. Lakini sera iko. Mimi nawasihi mabalozi na maafisa wengine wasikilize machache ambayo nitayaeleza. Yanaweza kuwa kama sera ya balozi zetu. La kwanza kabisa, tunataka kujivunia kuwa Wakenya. Nafikiria hilo ndilo jambo la kwanza kabisa katika sera ya balozi zetu. Wanakenya wajivunie kuwa Wakenya. Ni mambo mengi sana mema ambayo yamefanyika hapa ambayo yanataka Mkenya akiwa nje aweze kuwaelezea wale walioko ng'ambo. Tumekuwa wa kwanza katika Afrika kuleta elimu ya msingi bila malipo. Nakumbuka kwamba Rais mstaafu wa nchi ya Amerika, Bw. Bill Clinton, aliposikia jambo hilo, alisema kwamba mtu wa kwanza angependa kukutana naye ni Rais wa nchi ambayo imeleta elimu ya msingi bila malipo. Elimu ya msingi imekuwa shida sana katika nchi nyingi. August 29, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3577 Isitoshe, Bw. Naibu Spika wa Muda, sisi tumefufua uchumi ambao ulikuwa umezorota kwa miaka mingi. Tuko na makampuni kama Kenya Airways (KQ), KenGen, benki kama Equity na kadhalika, ambazo zimeonyesha kwamba Wakenya wanaweza, kwa kweli, kufaulu kwa mambo ikiwa wanajitahidi. Tunajua kwamba wakati huu, uchumi wetu sasa unapanda kwa kiwango cha asimilia 6. Hilo ni jambo ambalo sisi ni lazima tujivunie. Bw. Naibu Spika wa Muda, sote tumezungumzia juu ya ufisadi ambao ulikuwa katika nchi hii. La ajabu ni kuona kwamba kunao Wakenya ambao wanahamia kule ng'ambo. Wanakwenda kuongeza chumvi na kusema kwamba ufisadi umezidi katika nchi hii. Lakini ukweli ni kwamba, Serikali hii imepigana sana na ufisadi. Inaendelea kufaulu kuurudisha chini. Tunataka sisi tujivunie kuwa Wakenya. Hiyo ni sera ya mambo yetu ya kigeni. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa mara ya kwanza, Gross Domestic Product (GDP) imepita"
}