GET /api/v0.1/hansard/entries/206591/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 206591,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206591/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Awori",
    "speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
    "speaker": {
        "id": 290,
        "legal_name": "Moody Arthur Awori",
        "slug": "moody-awori"
    },
    "content": ". Ni nani angefikiria Kenya inaweza kufika kiwango hicho? Tuna wanariadha ambao wameleta sifa kubwa katika nchi hii. Nachukua fursa hii kuwapongeza watoto wetu walioko huko Osaka, Japan. Wametuletea medali tele. Kwa sababu ya wanariadha wetu, tukienda ng'ambo, lazima tujivunie kuwa Wakenya. Bw. Naibu Spika wa Muda, la pili katika sera hii ni kutafuta biashara. Tunataka kazi ya balozi zetu iwe ya kutafuta biashara. La kwanza ni kutafuta wawekezaji. Kuna sehemu nyingi sana ambazo zinataka wawekezaji, ili tuweze kuimarisha maisha. Kwa mfano, kawi. Viwanda vingi sana haviwezi kuendelea mbele bila kawi. Tungependa wawekezaji waweke rasilimali zao katika kawi ili iweze kuenea katika nchi hii. Hatua hiyo itapunguza gharama ya kufanya biashara hapa nchini. Tungependa pia wawekezaji waweke rasilimali zao katika sekta ya barabara ili wasimamie barabara kadhaa humu nchini. Hii ni njia moja ambayo itatusaidia sisi kwa usafirishaji wa watu na pia kuimarisha biashara yetu. Tungependa pia wawekezaji waje kutusaidia kuanzisha kampuni nyingi za usafiri wa reli kwa sababu kwa muda mrefu tumekuwa na shirika moja pekee. Tungependa pia waje kuweka rasilimali zao katika biashara ya kutengeneza mbolea, kwa sababu nchi hii inategemea ukulima kwa wingi. Tungependa pia wapanue bandari yetu ya Mombasa. Bw. Naibu Spika wa Muda, nakumbuka wakati Wajapan waliposhindwa vita vya 1945. Walijitahidi na kuhakikisha kwamba sera yao ya ubalozi itakuwa ni biashara na kuimarisha uchumi. Walituma watu wao katika nchi mbalimbali hasa Marekani, ili kuangalia na kuiga mienendo ya kuimarisha uchumi. Wakati huu, miaka 60 baadaye, Japan ni moja ya nchi duniani ambayo imeendelea sana katika biashara. Bw. Naibu Spika wa Muda, sera ya tatu ni sisi kusahihishana katika Afrika. Zamani tulikuwa na Shirika la Organisation of African Union (OAU). Shirika hilo lilikuwa linasema: \"Angalia tu jirani yako lakini usimwingilie hata akiwa anaharibu, kuua na kufanya mambo kadhaa mabaya.\" Ni furaha kwamba tumeondoka OAU na kuingia katika Muungano wa Afrika yaani Africa Union (AU) ambapo tunaweza kusahihishana tukifanya makosa. Hii ndio itatuwezesha sisi kuanza kuungana katika majimbo na nchi ili tuweze kuwa wengi. Wakati huu, mtindo unaofaa ni kuungana na watu wengi jinsi tulivyo katika Afrika Mashariki. Hii inawezekana ikiwa sisi tunaweza kukosoana. Ukimwona jirani yako akifanya mambo ambayo hayaambatani na heshima na kadhalika, inafaa umshawishi ili mkubaliane naye. Bw. Naibu Spika wa Muda, biashara inataka eneo kubwa. Tuna furaha kwamba katika Afrika Mashariki sasa tuko na idadi ya watu karibi 120 millioni. Hii itatuwezesha kupunguza gharama ya kutengeneza bidhaa na vifaa ili tufanye biashara katika soko la dunia. Bw. Naibu Spika wa Muda, sera ya nne ni sisi sasa kujitegemea. Tunataka kujitegemea kwa kulipa kodi na kutumia pesa zetu vyema. Tuwache kuomba kutoka nchi za nje kwa vile mwombaji ni mtumwa. Hii ndiyo inatufanya tudharauliwe. Ikiwa kila mmoja wetu ataweza kulipa kodi tunaweza kujimudu. Asilimia 93 ya Makadirio, mapato na matumizi ya pesa za Serikali ni pesa ambazo zimetoka hapa nchini. Tungependa hii iwe ni sera yetu ya ubalozi. Sisi wenyewe tunafaa kujitegemea. 3578 PARLIAMENTARY DEBATES August 29, 2007 Bw. Naibu Spika wa Muda, sera ya sera ya tano ni kutambua wale Wakenya wanaoishi katika nchi mbalimbali duniani. Hawa ni watoto wetu. Wakati huu tunaelezwa kwamba Wakenya karibu 100,000 wanaishi Marekani, Uropa na nchi zingine za Afrika. Inasemekana pia kwamba Wakenya hawa wanaleta Kshs67 bilioni nchini. Ikiwa wanaleta kiwango hiki cha pesa nchini wanastahili kuheshimiwa na kutambuliwa. Balozi za Kenya zilizoko katika kila nchi sasa zina jukumu la kuwatafuta Wakenya kokote waliko na kuwasajili. Hatua hiyo itahakikisha kwamba Wakenya wale wataweza kuisaidia nchi. Sera ya saba ni kumiliki mali yetu ilioko katika balozi zetu zilizoko nchi mbalimbali. Tungependa kumiliki mali yetu ilioko katika nchi hizo, kwa mfano, ofisi na nyumba za wafanyakazi wetu walioko huko. Ni rahisi sana kufanya hivyo kwa sababu riba katika nchi hizo iko chini sana. Kwa hivyo tunaweza kukopa pesa. Kwa haya machache, naunga mkono Hoja hii."
}