GET /api/v0.1/hansard/entries/206762/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 206762,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/206762/?format=api",
"text_counter": 78,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, Waziri Msaidizi amesema ya kwamba Serikali haina pesa za kutumiwa na kamati hizi za amani. Lakini Serikali inatekeleza mipango ambayo inahatarisha amani hapa nchini. Wanabuni wilaya bila kuweka mipaka maalum. Ninasikia kuna mpango wa kubuni wilaya mpya kutoka Wilaya ya Taita Taveta ambapo mipaka haijulikani itakuwa wapi. Jambo hili linaleta migogoro na migongano. Bw. Naibu Spika, je, Serikali itapata wapi pesa za kupambana na migogoro inayozusha kwa kubuni wilaya bila kuwa na mipaka maalum?"
}