GET /api/v0.1/hansard/entries/20679/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 20679,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/20679/?format=api",
    "text_counter": 253,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Yakub",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 378,
        "legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
        "slug": "sheikh-dor"
    },
    "content": "Asante Bwana Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono Hoja kwamba Kamati hii ili iongezewe muda na idadi ya wafanyakazi. Hii ni Kamati ambayo Wakenya wanaitegemea sana hasa wale ambao ni wakimbizi wa ndani ya nchi. Ningeomba kupitia kwa Mwenyekiti wao, wajaribu wafike maeneo yote, husuwan eneo la Lamu ambalo mwaka wa 1963 lilikuwa na vita vingi kutokana na kikundi cha shifta. Watu wa Lamu walitoroshwa kutoka maeneo yao na hivi sasa, hawana makao. Ningeomba Kamati hii ifike Lamu ili iwasaidie watu wa eneo hilo kutokana na vita vya shifta."
}