GET /api/v0.1/hansard/entries/207377/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 207377,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/207377/?format=api",
    "text_counter": 170,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Pia kuna \"janga\" linalowakumba wazazi wa watoto wanahudhuria shule za malezi. Mara nyingi wazazi huwa wanahangaika wanapotafuta namna ya kuwalipia karo watoto wao. Wakati mwingine, akina mama wanaofanya biashara ndogo ndogo, kama vile kuuza ndizi, wanahitajika kulipa Kshs300 kwa mwezi kwa kila mtoto. Katika muhula mmoja, mzazi hulipa Kshs900, jambo ambalo huwa linamtatiza. Licha ya hayo, waalimu hunyanyaswa kupita kiasi. Mshahara wanaolipwa na wazazi mwalimu wa shule hizo haupiti Kshs5,000 kwa mwezi. Wengi wa waalimu hao hulipwa mshahara wa Kshs3000 kwa mwezi. Miongoni mwa hao wanaolipwa Kshs3,000 kwa mwezi, hufanya kazi kwa zaidi ya miezi sita bila kulipwa cho chote. Kwa hivyo, Serikali inapaswa kuchukua jukumu la kuwalipa waalimu hao. Tumeifanya elimu ya msingi kuwa ya bure, lakini inafaa tufahamu kwamba tumejenga \"nyumba\" ambayo haina msingi bora. Sasa, tunafikiria kuweka msingi utakaokuwa bora kwa elimu humu nchini."
}