HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 207431,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/207431/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kingi",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 248,
"legal_name": "Joseph Kahindi Kingi",
"slug": "joseph-kingi"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoa mchango wangu kwa Hoja hii. Hoja hii ni muhimu sana, kwa sababu inahusu watoto ambao wameachwa na wazazi na sasa ni yatima. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumpongeza mhe. Prof. Mango kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Hoja kama hizi ambazo ni muhimu zinahitaji kuungwa mkono na weheshimiwa Wabunge wote. Nashangaa kwamba wengi wetu hawako Bungeni kana kwamba hili jambo ni la mzaha, na hali ni jambo ambalo linahitaji kupewa uzito sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, kila mahali katika Taifa hili utakapoenda, utapata vijana wengi ambao ni yatima na hawana msimamizi maalum. Wana matatizo mengi kuanzia ukosefu wa chakula hadi ukosefu wa karo na mahali pema pa kulala. Kwa ufupi, hawa ni watoto ambao wanaishi kwa matatizo makubwa sana. Ingawaje yako mashirika mengi katika nchi hii ambayo yamejitolea kuwasaidia watoto hawa, ukosefu wa kushirikisha kazi za mashirika haya 3364 PARLIAMENTARY DEBATES August 22, 2007 umesababisha watoto hawa kuendelea kupata shida kila wakati. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni wazi basi kwamba kuunda au kutenga rasilimali kutoka kwa mfuko wa Serikali, ambao labda utawekwa chini ya usimamizi wa sehemu za uwakilishi Bungeni, litakuwa jambo bora sana. Sehemu hizi za uwakilishi Bungeni kila siku zinakuwa sehemu imara kwa sababu matatizo mengi sasa yanaangaliwa kutoka sehemu zetu za uwakilishi Bungeni. Tutakapokuwa na rasilimali itakayowekwa chini ya usimamizi wa sehemu za uwakilishi Bungeni, itakuwa rahisi kuweka rasilimali hii chini ya kamati inayojumuisha sehemu zote za uwakilishi Bungeni. Kwa hivyo, itakuwa rahisi kupata au kuwatambua watoto hawa ambao ni yatima ili tuweze kuwasaidia. Tutaweza kuwatafutia shule bora, mahali pa kulala, mavazi na hata matibabu wakati wanapougua. Kwa jumla, tutaweza kuwasimamia na kuhakikisha kwamba wao pia wanaishi maisha bora kama watoto wengine. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo, mimi ninaunga mkono Hoja hii. Naamini kwamba itakapopita, Wizara inayohusika na swala hili italishughulikia vilivyo ili tuhakikishe kwamba watoto wetu wanaendelea kupata maisha mazuri. Kama walivyosema wenzangu, watoto wetu ndio taifa letu la kesho. Kwa hivyo, tunahitaji kuweka msingi bora ili tuweze kupata viongozi na wafanyakazi watakaoweza kusaidia taifa letu. Wakati tunapofanya hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba chanzo au sababu ambazo zinaweza kufanya jamii zikapotea ndipo watoto wetu waweze kuwa yatima, zinapunguzwa iwezekanavyo. Hii ni kwa sababu hatutaki taifa litakalojaa watoto yatima kutokana na tabia ambazo tunaweza kuziepuka. Leo hii tunakubaliana kwamba chanzo kimoja ambacho kinasababisha watoto wengi kuwa yatima ni ugonjwa wa UKIMWI. Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba katika kazi zetu na shughuli zetu za kila siku, tunaangazia aina ya tabia ambazo zinaweza kusabisha magonjwa kutapakaa. Kuna tabia moja ambayo watoto wengi wemejiingiza ndani. Tabia hiyo ni ya kunywa pombe haramu na kutumia madawa ya kulevya. Mara nyingi, tabia kama hizi zinaweza kuelekeza jamii yetu kupata magonjwa kama UKIMWI. Baadaye, hata wazazi pia wanaweza kupoteza maisha yao. Kwa hivyo, ni lazima tuelekeze nguvu zetu na uwezo wetu kuhakikisha kwamba tunaondoa mambo kama haya katika taifa letu ili watoto na wazazi wetu waweze kuishi maisha mema bila matatizo. Katika shule zetu, ni lazima tuhakikishe kwamba tabia ambazo zinaweza kusababisha magonjwa mengi kama haya, zinaondolewa ili watoto wasome vizuri. Bw. Naibu Spika wa Muda, tuna vyombo vingi vya habari katika taifa letu. Tuna magazeti, stesheni za televisheni, redio na kadhalika. Tungeomba vyombo hivyo vya habari vitusaidie katika taifa hili, kwa kueneza hatari za magonjwa kama UKIMWI. Pia vieneze hatari za ulevi kwa sababu mambo kama haya mara nyingi husababisha ajali na kufanya watoto wetu kuachwa bila wazazi, na hivyo kuwafanya mayatima. Wakiwa hivyo, wanaweza kujiingiza katika mambo ambayo si mazuri katika maisha yao. Bw. Naibu Spika wa Muda, tukiwatunza watoto wetu vizuri, wanaweza kuwa wachezaji wazuri wa taifa hili. Wanaweza kuwa wanasanaa na waimbaji wazuri. Wanaweza kufanya shughuli nyingi ambazo zitawaletea fedha na waishi maisha mazuri. Kwa hivyo, ni juhudi yetu, kama taifa, kuhakikisha kwamba tunawalinda watoto yatima kwa kutenga rasilmali za kitaifa kutatua matatizo yao, ili waweze kuendelea na maisha kama watoto wenzao. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga Hoja hii mkono, na kumpogeza tena, Profesa Mango, kwa kuileta mbele ya Bunge."
}