GET /api/v0.1/hansard/entries/207610/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 207610,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/207610/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kingi",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 248,
"legal_name": "Joseph Kahindi Kingi",
"slug": "joseph-kingi"
},
"content": " Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuzungumza mambo machache kuhusu Hoja hii muhimu sana inayohusu mambo ya maji kwa taifa letu. Nataka kuunga mkono wenzangu ambao wamempongeza Waziri pamoja na maofisa wake kwa kazi yao nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika taifa letu. Miaka michache iliyopita, taabu ya maji ilikuwa kila mahali; hata huko kwetu sehemu za Kilifi na Ganze, wananchi walikuwa na matatizo sana. Katika wakati wa ukame, wananchi walikuwa wakitembea kilomita nyingi wakitafuta maji ambayo kwanza hayakuwa masafi na yalikuwa yakiwapatia shida za ugonjwa mara kwa mara. Tunataka kushukuru Wizara hii kwa sababu imesambaza maji katika sehemu nyingi za taifa hili. Huko kwangu, tulikuwa na sehemu kama zile za Bamba, Vitengeni na Ganze ambapo wananchi walikuwa wakipata shida sana. Wizara ilirekebisha laini ya maji inayotoka sehemu ya Silala kuenda Bamba. Wamejenga tangi za maji na kutoka hapo, wanasambaza maji hata vitongojini. Tunataka kusema kwamba hiyo ni kazi nzuri inayoendelea. Tuna imani kabisa kwamba kama Wizara hii itapatiwa pesa katika wakati ujao, basi, taabu ile imekuwa ikiwakumba Wakenya, bila shaka, itakuwa imemalizika. Wanapopewa fedha zaidi watakuwa na uwezo wa kujenga hata mabwawa makubwa zaidi ya yale tuliyonayo. Pia wataweza kununua vifaa zaidi vya kupima au vya kutafutia maji yale ambayo yako chini ya ardhi ili tuweze kujenga visima vingi zaidi. Tunatarajia kwamba hivi karibuni, ndoto ile tumekuwa nayo ya kwamba kutakuwa na laini ya pili ya Chemichemi ya Mzima itatimia. Kwa sababu tukiwa na laini ya pili ya kutoka Mzima kwenda Mombasa basi matatizo ya maji ambayo hukumba mji wa Mombasa, mara kwa mara, yatapungua. Tunatarajia pia kwamba Wizara itaongeza laini ya pili kutoka sehemu za Malindi na Lango Baya na ipitie Bamburi ifike Mombasa ili watu wa Mombasa waweze kuwa na maji ya kuwatosha. Wakati wanapoongeza laini hizo mbili, basi, watakumbuka kuwasambazia maji zaidi wananchi wanaokaa katika sehemu za barabara hizi au sehemu ambazo laini hizi zitapitia."
}