GET /api/v0.1/hansard/entries/207612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 207612,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/207612/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kingi",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker": {
        "id": 248,
        "legal_name": "Joseph Kahindi Kingi",
        "slug": "joseph-kingi"
    },
    "content": "Nakubaliana na wenzangu ambao wanasema kwamba Serikali haijafanya utafiti ambao utatuwezesha kuhifadhi maji mengi ambayo yanapotea wakati mvua inaponyesha. Wakati mvua inaponyesha, tunapoteza maji mengi. Maji mengi hupotea kwa sababu hatujatengeneza mabwawa ambayo yanaweza kutumiwa kuteka na kuhifadhi maji hayo ambayo yanayoweza kutumika katika shughuli za kilimo, mifugo na shughuli zingine nyingi. Kuna sehemu moja huko kwetu, Rare, ambayo nina hakika uchunguzi ukifanywa, maji mengi yanayopotea katika bahari yataweza kuzuiliwa hapo ili tuweze kufanya shughuli zinazohusiana na mambo ya kilimo. Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono wale wanaosema kwamba Wizara hii imefanya kazi nzuri katika kuboresha mambo ya maji. Maji sasa ni masafi na magonjwa mengi ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi ambayo husababishwa na maji machafu yamepungua. Tunapongeza Waziri kwa kazi nzuri na kushawishi Wizara iendelee kufanya kazi hiyo nzuri. Tunamatumaini kwamba Serikali itaiongezea Wizara hii fedha ili iendelee kueneza shughuli za maji. Bw. Naibu Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hiyo. August 22, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3389"
}