GET /api/v0.1/hansard/entries/207653/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 207653,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/207653/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kupata nafasi hii, na namshukuru Waziri kwa kunipatia hizi dakika chache ili nipate kutoa sauti yangu. 3402 PARLIAMENTARY DEBATES August 22, 2007 Sehemu ninayotoka ni kame, na ninachomwomba Waziri tu ni kwamba apate wasaa wa kuzuru Kinango ajionee, kwa sababu hata nikizungumza hapa, pengine hatutapata suluhisho la kudumu. Hivi sasa mji wa Kinango unapata maji katika siku kumi kati ya siku 30; kwa siku 20 hatuna maji, na tuna hospitali kuu katika mji huo. Naomba kutafutwe njia mwafaka ya kujua mji wa Kinango utapata maji kwa njia gani. Pili, naishukuru Wizara kwa sababu imejaribu kutafuta mikakati ya kuwasaidia wale watu ambao hawajiwezi kwa kuwachimbia dam katika sehemu yangu. Lakini nataka nimwaambie Waziri kuhusu Mwakunde Dam . Mwanakandarasi alipewa kazi, hakuimaliza na amevichukua vifaa. Sasa hatujui hatima ya dam ile ni nini. Pili, mwandakandarasi alipewa kazi ya Gede Dam, hakuimaliza na hakuna chochote kinachoendelea. Wananchi hawajui ni kitu gani kinachoendelea katika ile sehemu. Twaomba tu Wizara ipate kuchunguza na kujua ikiwa mwanakandarasi huyo ana vifaa na uwezo wa kufanya ile kazi ama hawezi. Mwisho, tegemeo letu katika mji wa Kinango ni Nyalani Dam, na tumekuwa tukiona katika magazeti kwamba ingeshughulikiwa. Kama Serikali ingeweza kutenga pesa na kujaribu kuipanua Nyalani Dam, mifugo wetu wangeweza kusitirika na kutoka katika ile shida inayowakumba. Namshukuru Waziri na Katibu Mkuu katika Wizara kwa sababu mambo fulani fulani yameanza kuwa na mabadiliko. Lakini ninachoomba ni kwamba sehemu hizi zishughulikiwe. Nikimalizia, ni kwamba Waziri atafute nafasi yeye mwenyewe aizuru sehemu yangu ili nikizungumza wananchi wawe wanamjua muhusika na kazi inayokusudiwa kufanyika. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga mkono na Mungu awape umri."
}