GET /api/v0.1/hansard/entries/207962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 207962,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/207962/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nitoe maoni machache kuhusu hii Hoja ya Wizara ya Maji na Unyunyizaji Maji Mashamba. Kwanza, nitaungana na wenzangu kuipa pongezi Wizara hii kwa kazi inayoifanya katika taifa lote. Lakini, kule Wundanyi, hatujaona mkono wowote wa Wizara hii. Mbali na kuleta Maswali mengi katika hii Bunge kuhusu Ngilinyi dam, Kakimwaisa Water Project na mradi wa Kishushe, pia kuenda kwa Wizara na barua nyingi ili kuwakumbusha na kumkumbusha Waziri hapa, na hata Waziri kuahidi katika hii Bunge, hakuna hata ahadi moja ambayo imetekelezwa na Wizara hii katika sehemu ya uwakilishi ya Wundanyi. Lakini wakati huu, tunaomba tuone mkono wa Wizara hii katika Wundanyi. Tumefanya miradi mingi ya maji kupitia pesa za mfuko wa maeneo Bunge. Karibu nusu ya bajeti yetu ya pesa za mfuko wa maeneo ya Bunge imeenda kwa maji. Vile vile, sehemu kubwa ya Wilaya ya Taita-Taveta, na Wundanyi Constituency pia, ni eneo kame. Kwa hivyo, tungeomba kwamba lokesheni ya Kishushe, ambayo ni sehemu kame katika Wilaya ya Taita Taveta, na ambayo iliingizwa katika orodha ya zile sehemu ambazo zitafaidi kutokana na Water Trust Fund, iangaliwe. Tunaomba Wizara itufikirie sana kwa njia hiyo. Baada ya kusema hayo, Bw. Naibu Spika wa Muda, ningeomba kuongeza kwamba kile kitu ambacho ningetaka kukiona kama Mkenya--- Kwa sasa, tunafikiria kwamba tumefaulu sana na tungetaka hakikisho litolewe na Wizara hii kwamba maji yote tunayokunywa mijini, hasa Nairobi na mitaa ya mabanda, yako salama kwa kunywa. Nafikiri juhudi nyingi za hiyo bajeti--- Ninaiunga mkono bajeti hii. Hata ingeongezwa iwe wingi zaidi kwa sababu maji ni muhimu sana. Sehemu kubwa ya bajeti hii pia inafaa itumiwe kuhakikisha kwamba maji tunayoyaweka ni masafi na yako salama kwa kunywa. Vile tunavyoendelea sasa, watu wanaofaidika na maji ni wale ambao wako na pesa. Hao watu wananunua maji yale ambayo yanauzwa. Tunaona kwamba kama nchi, tunakubali hali hiyo ya ubepari na ubeberu. Hata kampuni kutoka nje zinakuja na kuuza maji ndani ya nchi yetu. Hilo ni jambo ambalo haliwezi kufikirika. Ni uwekezaji wa namna gani huo wa kukubali kampuni ya Coca Cola kuingia na kuanza kuuza maji ndani ya nchi yetu? Kwangu mimi, hiyo ni dalili kubwa sana ya ukoloni mambo leo, ambao ni lazima tupambane nao kama taifa. La muhimu 3312 PARLIAMENTARY DEBATES August 21, 2007 ni kwamba, ni lazima tuhakikishe kwamba tukifanya miradi, inawafikia watu kwa usalama. Naomba pia kuunga mkono wale ambao wamesema - wakiongozwa na Prof. Wangari Maathai - kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati ya maji na mazingira. Nafikiri huo ni ukweli mkubwa kabisa. Tukilinda mazingira yetu, tutaongeza maji. Vile vile, tukiongeza maji, wananchi watakuwa na motisha sana kuhifadhi mazingira. Pia, naomba kuchukua fursa hii kupongeza Baraza la Jiji la Nairobi kwa juhudi ambazo zinaonekana za kupanda miti katika Mji huu. Hiyo ni juhudi ya kupongezwa sana. Kama miji mingine katika nchi yetu ingefuata mfano wa Baraza la Jiji la Nairobi, nafikiri baada ya muda mrefu, tungeleta mandhari mazuri sana katika nchi yetu kwa upande wa mazingira. Mfano wa uhusiano wa mazingira na maji ni kwamba Milima ya Taita-Taveta ni sehemu ya Kenya ambayo ni nzuri sana kimandhari. Ni sehemu ambayo inataka kulindwa vizuri sana kwa vizazi vya sasa na vile vijavyo. Kama tungetoa maji kutoka Mzima Springs na kuyapeleka sehemu za nyanda za chini za Taita-Taveta, wananchi wengi wangeteremka kutoka milimani na kuja kulima huko chini. Kule juu, kungebaki kama zamani. Kungepandwa msitu. Kungekuwa na misitu mikubwa sana. Vile vile, baada ya miaka 15 au 20, tungeanza kuona maji yakitiririka kutoka milima ya Taita-Taveta. Kwa hivyo, jambo ambalo tunaomba kutoka kwa Wizara hii ni kwamba, huo mradi wa maji wa Mzima Springs--- Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna maji mengi sana katika Mzima Springs ambayo yanatiririka mpaka huko Bahari Hindi. Kama kungekuwa na mradi wa maji wa Mzima Springs na pesa zitengwe kupeleka maji sehemu za Kishushe, Mlilo, Ngulia, Mboldo na sehemu zingine za Mwakitau na nyanda za chini za Taita-Taveta, sio tu tungeongeza lishe na chakula katika Wilaya ya Taita-Taveta, lakini vile vile, tungepeana motisha ya kulindwa kwa mazingira. Wananchi wanaofinyana katika milima ya Taita-Taveta wengeteremka chini na kuanza kulima huko chini. Pia, maji yataanza kutiririka kutoka huko juu. Kwa hivyo, tunaomba hii Serikali itekeleze mradi huo kwa sababu utazalisha mazao katika Mkoa wa Pwani. Hata sehemu nyingine za Ukambani zitafaidika kutokana na mradi huo wa Chemchemi ya Mzima. Huu mradi ni mkubwa sana na ukitekelezwa, utaleta maendeleo makubwa. Utasaidia sana katika kuendeleza sehemu hiyo ya nchi yetu. Ni mradi ambao wananchi wa Taita- Taveta wamekuwa wakiulilia kwa muda mrefu sana. Wananchi wa Taita-Taveta wanasikitika sana kwa sababu maji kutoka Chemchemi ya Mzima ni mengi sana na huteremka hadi Mombasa. Yanapofika huko, maji hayo huuzwa na Baraza la Jiji la Mombasa ilhali wao wenyewe hawafaidiki na chochote. Hata sasa, kuna tatizo kubwa sana la maji kule Voi. Tunaomba Wizara ya Maji na Unyunyizaji, katika Bajeti hii, itenge pesa nyingi sana ili iweze kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji. Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, kuna taasisi nyingi sana na mamlaka mengi ambayo yameundwa na Wizara ya Maji na Unyunyizaji. Haya ni mabadiliko ambayo yameletwa na Wizara hii. Lakini haya mabadiliko wakati mwingine huleta urasimu mkubwa sana mpaka tunashindwa la kufanya. Kwa mfano, huko Taita Taveta, huwa tunaambiwa tuchukue baadhi ya leseni huko Machakos. Kutoka Wundanyi hadi Machakos ni mamia ya kilomita. Wananchi hawajaelewa jambo hili na hawawezi kuelewa. Ni sharti urasimu uondolewe ilhali irahisishwe na fedha zitumike katika kuboresha uenezaji maji katika kila sehemu. Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, tunataka Wizara ya Maji na Unyunyizaji, katika wilaya zote isimamiwe vizuri sana kwa maana hapo ndipo kuna ufisadi mkubwa. Ni lazima Wizara ifuatilie jambo hilo. Miradi mingi imekwama kwa sababu ya ufisadi ulioko mashinani. Hata miradi ya hazina ya CDF imekwamishwa kutokana na ufisadi unaopatikana katika Wizara ya Maji kule mashinani. Lazima Wizara hii ichukue hatua madhubuti ikiwa tunataka kufaulu kutumia haya mabilioni ya pesa kuongeza maji zaidi. Kipimo cha maendeleo katika nchi ni kwamba tusirudie kufanya mambo yale yale. Kesho ikifika, tuwe tumesonga hatua mbele zaidi katika kutatua tatizo la ukosefu wa maji wala si kukwamishwa kwa August 21, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3313 sababu ya ufisadi. Jambo ninalosisitiza ni kwamba tatizo kubwa katika kutotekeleza miradi ya maji ni ufisadi. Ikiwa Waziri atakabiliana na tatizo la ufisadi katika mashinani, basi atapiga hatua kubwa mbele katika kutekeleza miradi ya hii Wizara. Malalamiko mengi yanatokana na ufisadi; mpaka hawana haya! Katika pesa ambazo tunatoa kutoka hazina ya CDF, yaani Kshs2 milioni, Wizara ya Maji na Unyunyizaji huitisha Kshs400,000. Kwa hivyo, lazima tuwe na sera maalum ya kuhakikisha kwamba hilo tatizo linatatuliwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo maneno machache, ningependa kuunga mkono hii Hoja ya Wizara ya Maji."
}