GET /api/v0.1/hansard/entries/208192/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 208192,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/208192/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi ili niongeze sauti yangu juu ya Hoja hii ya kwenda likizoni. Kusema ukweli na uwazi bado kuna kazi nyingi sana ya kufanywa. Kwa mfano, Wizara ya Ardhi ina kazi nyingi ya kufanya. Kwa hivyo, kusema Waziri aende kupumzika kwa muda wa wiki mbili ni hasara kwetu sisi na Kenya nzima kwa jumla. Lile ambalo Waziri angetangulia kulifanya ni kuyaleta marekebisho katika Wizara hii. Kwa mfano, angeweza kushughulikia swala la uchoraji ili nyumba zetu ziwe safi na zipangwe kwa utaratibu. Pia Wizara ya Maji bado ina kazi nyingi ya kufanya. Kwa hivyo, tukifunga Bunge hili na kwenda kupumzika, kazi hizi zote zitasimama."
}