GET /api/v0.1/hansard/entries/208222/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 208222,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/208222/?format=api",
"text_counter": 210,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Rai",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, tumechaguliwa kufanya kazi kwa miaka mitano. Wakati umefika wa sisi Wabunge kuongezewa muda wa kufanya kazi katika Bunge hili. Haifai sisi kushurutishwa kwenda nyumbani wakati matatizo yamezidi katika sehemu zetu. Bw. Naibu Spika, katika historia ya taifa hili ni mara ya kwanza mwaka huu hatujamaliza Hoja inayoshughulikia Bajeti ya Wizara mbalimbali. Kufikia wakati huu, si Wizara nyingi ambazo zimepata pesa. Leo tunaombwa kwenda nyumbani wakati Wizara nyingi hazijapata pesa za kuziwezesha kufanya kazi. Bw. Naibu Spika, hii ni dhambi kubwa. Wakati kama huu, tunahitaji sisi kama Wabunge kulaani vitendo kama hivi. Kama kuna baadhi ya Wabunge ambao wanajisikia wamechoka, basi wana uhuru wa kujiuzulu kwa sababu kazi hii si ya lazima. Watuwache sisi tunaotaka kuendelea na kazi. Muda si mrefu, tutafanya uchaguzi mkuu. Hatutishwi na uchaguzi. Tuko tayari hata kama Bunge litavunjwa kesho!"
}