GET /api/v0.1/hansard/entries/208226/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 208226,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/208226/?format=api",
    "text_counter": 214,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ni lazima tuseme ukweli. Ninakumbuka yuko nabii mmoja ambaye alikuwa na umri wa juu na akajisikia kuchoka. Akaenda akaomba radhi apate kuondoka duniani lakini akaambiwa wakati wake haukuwa umefika. Aliambiwa asubiri hadi nabii fulani aje kwanza amuone ndio yeye aombe radhi ya kuondoka duniani. Umri wetu wa kuishi hapa Bungeni haujamalizika. Kwa hivyo, kukatiwa maisha yetu, haiwezekani. Bw. Naibu Spika, kama Serikali ina wakati, ikajipange, ijiandae na ijue kwamba sisi tuko tayari kufanya kazi na kuendelea kumpa huduma mwananchi anayesubiri huduma kule nje. Bw. Naibu Spika, napinga vikali na moja kati ya mambo ambayo yanaudhi ni kama vile ulivyomsikia Bw. Ojode akizungumza pale. Kule kwetu Pwani, kuna shamba moja linaitwa Vipingo, ambalo lilikatwa, na watu walipokaa katika Land Control Board, walikataa. Lakini DC wa wakati huo akakata shauri kwamba lazima shamba hilo litoke na hivi sasa, limefanywa VipingoGolf Ridge . Mambo kama hayo ni mambo ambayo yananyanyasa hadhi ya Serikali!"
}