GET /api/v0.1/hansard/entries/208468/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 208468,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/208468/?format=api",
    "text_counter": 108,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, swala hili kuhusu watu wanaopewa kandarasi za barabara ni muhimu na la kitaifa. Nimeshindwa kuelewa uhusiano uliopo kati ya Wizara na wanakandarasi wa barabara. Kandarasi nyingi zinapewa watu ambao hawafanyi kazi. Kwa mfano, barabara ya Thika ambayo Mhandisi Toro anaitumia anapoenda katika eneo lake la uwakilishi la Bunge, imejengwa kwa mwaka mzima ingawa ni kazi ndogo. Kuna barabara nyingine ambayo ilipewa kandarasi kutoka Musau-Windanyi-Verunga; barabara ya Bura. Sehemu ya Mulondo imejengwa na slab na imebomoka kabisa. Wizara inajua jambo hilo lakini haifanyi lolote. Je, wana uhusiano gani na wanakandarasi? Kwa nini mnawaogopa?"
}