GET /api/v0.1/hansard/entries/209873/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 209873,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/209873/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuunga mkono Hoja hii. Hoja hii inaangazia tatizo lenyewe. Lakini swala la msingi ni kuondoa huu mfumo wa ubepari. Nchi hii ni tajiri kabisa. Inaweza kupatia kila mtu elimu ya bure katika shule za upili. Lengo la Serikali hii sasa--- Elimu inaongeza pengo kati ya watoto matajiri na watoto maskini. Tusipobadilisha jambo hilo, hata tukiongeza huu mfuko, tatizo hilo litaendelea. Kwa hivyo, naunga Hoja hii mkono kwa sababu inaonyesha tatizo hilo. Tatizo la msingi ni kupambana August 8, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3031 na sera ya ubepari ambayo imekuwako tangu tupate Uhuru hadi sasa. Nchi hii ni tajiri, lakini rasilmali hazitumiwi kwa ajili ya watoto maskini. Zinaendelea kutumiwa kwa ajili ya watoto matajiri. Kuna shule za matajiri na zile za maskini. Tusipotatua jambo hilo, haya mengine yote tutakuwa tunafukuza upepo. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}