GET /api/v0.1/hansard/entries/209876/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 209876,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/209876/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuunga mkono Hoja hii ya ushuru wa elimu, ambayo itawasaidia vijana wanaotoka katika jamii maskini kuweza kuendelea na masomo yao. Bw. Naibu Spika wa Muda, tuko katika harakati ya kujenga nyumba ambayo haina msingi thabiti. Ningeonelea vyema ikiwa baadhi ya fedha hizo zitatumika kwa elimu ya malezi. Elimu ya malezi ndio msingi wa elimu hapa nchini, lakini kufikia hivi sasa, utakuta kwamba akina mama ndio wanaopata shida kwa sababu wanalipa karo kwa watoto wa nursery . Ikizidi sana, utakuta mwanafunzi analipiwa Kshs300 kwa mwezi; jambo ambalo akina mama hawawezi kamwe! Ingekuwa bora iwapo elimu ya nursery ingekuwa bure ili kila mtoto aweze kupata msingi bora na mwishowe, tutapata raia ambao wana misingi mizuri ya kielimu. Hatimaye, hata elimu ya bure katika shule za upili pia ina maana kwa sababu itawezesha wanafunzi wetu waendelee kielimu. 3032 PARLIAMENTARY DEBATES August 8, 2007 Pia, vile vile, tukisema kuwa karo ya shule za upili imeondolewa, tutakuwa bado hatujasema kitu kwa sababu karo hiyo ni ndogo sana kulingana na zile hela zinazolipwa. Kwa mfano, kwa mwaka, mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Mangu anahitajika kulipa Kshs53,000."
}