HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 209886,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/209886/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 253,
"legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
"slug": "mwandawiro-mghanga"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mimi naomba kuunga mkono hii Hoja ya maana sana. Nasikitika ya kwamba Waziri ya Mipango na Maendeleo na Waziri wa Fedha hawako hapa. Pia, wataalamu kutoka Wizara wa Mipango na Maendeleo na ile ya Fedha hawako hapa. Hii Hoja inalenga kusaili sera za kiuchumi za nchi hii. Imeletwa na mtu August 8, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3035 ambaye alikuwa Waziri wa Mipango na Maendeleo katika nchi hii. Vile vile, imewasilishwa na Dr. Awiti ambaye ni mtaalamu wa maswala ya kiuchumi. Dr. Awiti ana historia kali ya mapambano ya kukomboa hii nchi ili tupate maisha bora katika nchi yetu. Yeye amesafiri sana. Kwa hivyo, hii Hoja imeletwa na mtu ambaye ana maono kamili kwa nchi yetu. La muhimu zaidi ni kwamba wakati tunatekeleza hizi sera za ubinafsishaji--- Nimewahi kusema katika hii nchi yetu kwamba sisi Waafrika na Wakenya tutaanza kuendelea wakati tutajikomboa kimawazo. Ni wakati ambapo tutaanza kufikiria sisi wenyewe, tutazame jiografia ya nchi yetu, rasilmali zilizoko, mali ya asili na watu. Tukitazama historia ya majirani wetu na ulimwengu, na tufanye mipango yetu sisi wenyewe ambayo imezaliwa hapa hapa nyumbani, ndio Mwaafrika ataweza kuendela. Sisi pia tutaendelea. Lakini tukiendelea kusema kwamba tutaendelea kutegemea sera za kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na hata zingine zinazotoka Marekani na Uingereza kupitia kwa mashirika ya kibeberu na kibepari-- - Iwe ni Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Shirika la Biashara la Dunia. Ikiwa tutaendelea kutegemea sera hizo, tutaendelea kukwama na kuyumbishwa yumbishwa. Mara, uchumi unakua kwa asilimia 5 au 6. Mara, tunarudi nyuma! Kukua kwenyewe hakutafaidi maendeleo katika nchi yetu. Tunajua kwamba sera ya ubinafsishaji ambayo inatekelezwa kwa shauku kubwa katika nchi yetu inatokana na sera za kifalsafa za kipebari. Lengo la sera za kifalsafa za uchumi wa kipebari ni kuwafanya matajiri waendelee kuwa juu. Vile vile, lengo la falsafa ya kibepari katika nchi yetu, na Afrika kwa jumla, ni kuendelea kuipiga vita sarafu ya dola isiwe na nguvu na watu binafsi ambao ni matajiri wawe na nguvu ili waendelee kuamua mambo kuhusu nchi za Afrika. Hata sasa sarafu ya dola imekuwa si kitu! Kazi ya sarafu ya dola ni kuangalia mabepari tu wakiwanyanyasa watu na kunyonya nchi na hata kushirikiana na watu wa nje ilhali wafanyakazi na umma ukiendelea kutegemea watu binafsi katika nchi yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia historia ya uchumi wa nchi yetu, utaona kwamba kutoka mwaka wa 1960 mashirika ya umma yalikuwa yakifanya vizuri sana. Hata sasa, hakuna ushahidi madhubuti kuonyesha kwamba mashirika ya umma hayawezi kufanya kazi vizuri na kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Isitoshe, matatizo yanayosababisha mashirika haya kushindwa kufanya kazi yanaeleweka. Baadhi ya hayo matatizo yanatokana na ukabila, uingiliaji mwingi wa Serikali katika shughuli za mashirika hayo na kutokuwa na wataalamu ambao wana ujuzi wa kutosha katika mashirika yanayohusika. Kwa hivyo, tatizo si kwamba mashirika ya umma hayawezi kupata faida na kuendeleza uchumi wa nchi yetu. Tatizo ni kwamba kuna sababu nyingine tofauti ambazo zinasababisha haya yote kuwepo. Bw. Naibu Spika wa Muda, pamoja na hayo, imeonekana wazi kwamba kila kunapokuwa na ubinafsishaji katika nchi, watu hupoteza kazi zaidi. Vile vile, umaskini huongezeka zaidi katika nchi. Ubinafsishaji wa mashirika ya umma husaidia kuongeza pengo kati ya matajiri na maskini. Hii ni kwa sababu wanaonunua hisa katika mashirika hayo ni watu ambao tayari ni mabepari au matajiri na watu kutoka nchi za nje. Kwa hivyo, hata uhuru wa kiuchumi wa nchi hupunguka zaidi kila kunapokuwa na ubinafsishaji. Vile vile, manufaa yanayoambatana na kuwepo kwa mashirika ya umma, kwa mfano, kuwa na ujuzi na maendeleo zaidi, hudidimia zaidi. Bw. Naibu Spika wa Muda, madai ya kusema kwamba sekta ya kibinafsi haiwezi kuendeleza nchi hayathibitishwi na ukweli. Maendeleo katika nchi yanategemea mipango halisi iliyoko katika nchi. Kwa mfano, ukilinganisha nchi ya Libya na Nigeria ambazo zote zina mafuta, utagundua kwamba huko Libya, sarafu ya dola ina nguvu zaidi katika kudhibiti mauzo ya mafuta. Ndiyo maana kuna manufaa zaidi kwa wananchi na maendeleo mengi yanayotakana na mafuta katika nchi ya Libya kuliko ilivyo huko Nigeria ambako mafuta yanatawaliwa na mashirika ya mafuta ya dunia nzima pamoja na mabepari wa Nigeria. Mafuta hayo hayajawahi kusaidia wananchi wa Nigeria. Ukiangalia huko Latin America, kabla ya ndugu Hugo Chavez kuchukuwa mamlaka kupitia mapinduzi ya kisosholisti, wakati huo, mafuta yalikuwa yanatajirisha tu matajari wa Venezuela na mabepari wa huko Marekani na sehemu nyingine. Wananchi wenyewe wa 3036 PARLIAMENTARY DEBATES August 8, 2007 Venezuela hawakuwa wanafaidika na umaskini ulizidi. Leo hii, wakati ambapo Serikali imeingilia mambo hayo na sarafu ya dola kudhibiti uchumi wa mafuta, umaskini katika nchi ya Venezuela unazidi kupungua kwa kasi sana miongoni mwa watu wengi na nchi hiyo inaendelea kwa kasi zaidi. Venezuela sasa inasaidia nchi nyingine, kwa mfano, Cuba, Argentina na nyingine nyingi huko Latin Amerika kuendelea kwa sababu ya mafuta. Isitoshe, hata Kenya na nchi nyingine zimefaidika kwa sababu Serikali ya Venezuela sasa inadhibiti mauzo ya mafuta. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunajua kwamba katika nchi ya Cuba, ambako uchumi ni wa kisoshalisti na unatawaliwa na sarafu ya dola, kuna manufaa mengi. Duniani kote, ukichunguza nchi ambazo zinasemekana zinaendelea, pamoja na matatizo ambayo yanayozikumba nchi hizo, utagundua kwamba Cuba, ina manufaa mengi sana. Tunaweza kusema kwamba Cuba ni nchi huru zaidi na inatawala uchumi wake bora zaidi. Cuba ina manufaa makubwa kwa wananchi wake hasa kuhusu maswala yanayotusumbwa kama vile elimu ya bure kwa kila mtu. Huko Cuba, elimu kutoka shule ya nasari mpaka chuo kikuu ni ya bure kwa kila mtu. Vile vile kuhusu utawala wa ardhi, nyumba na barabara, nchi ya Cuba imeendelea sana kwa sababu imeweza kudhibiti uchumi wake kwa kutumia nguvu za sarafu ya dolar. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika wa Muda, ni muhimu kuunga mkono hii Hoja kwa sababu inawataka Wakenya kufanya utafiti kabisa kuhusu nchi yao kabla hawajaanza kutekeleza sera za kiuchumi hasa zile ambazo zinalenga kubinafsisha mashirika ya umma. Tujiulize, \"Je, ni kweli kwamba mashirika ya umma humu nchini hayawezi kuendelea?\" Vile vile tujiulize, ikiwa hatuwezi kuwa na sekta tatu, yaani sekta ya dolar, sekta ya vyama vya ushirika na sekta ya kibinafsi, je, sekta hizi haziwezi kuwepo wakati mmoja? Je, ni lazima tubinafsishe kila kitu na kuifanya nchi hii iwe ya mabepari? Ubinafsishaji wa mashirika ya umma una manufaa gani? Nilimwuliza swali Waziri wa Fedha humu Bungeni, wakati huo alikuwa mhe. Mwiraria, atueleze ni kazi gani zimeongezeka katika nchi yetu tangu tuyabinafsishe mashirika ya umma. Alishindwa kujibu! Hii ni kuonyesha kwamba hakuna utafiti wa kutosha. Ni lazima tuunge mkono hii Hoja kwa sababu inatuhimiza tufanye utafiti wa kisayansi na tuwahusishe wataalamu wetu kutoka vyuo vikuu na wasomi wengine wanaofanya utafiti. Tunataka Mawaziri wasome maswala ya kiuchumi siyo kutekeleza tu--- Shida nyingine ambayo nimeona ni kwamba watu, wakiwemo Mawaziri, hawasomi. Wao wanakaa tu! Wanatekeleza sera ambazo zinatengenezwa huko Washington ama Ufaransa. Kuna vitabu vingi vya uchumi na utafiti mwingi umefanywa kuhusu sera za kiuchumi, lakini wao ni wepesi wa kupokea mambo ambayo yanaletwa na Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) badala ya kujaribu kuzua suluhisho la matatizo yetu ya kiuchumi kutoka papa hapa nyumbani. Hii ndiyo sababu tunatakiwa kuunga mkono hii Hoja ili kabla hatujabinafsisha shirika lolote la umma, tulichunguze kisayansi na kutambua kama kweli shirika hilo limeshindwa kuleta faida ama ni kwa sababu linapata faida zaidi ndiposa mabepari katika nchi na nje wanalitaka. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo maneno machache, mimi naomba kuunga mkono Hoja hii."
}