GET /api/v0.1/hansard/entries/209909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 209909,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/209909/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii na nampongeza Dkt. Awiti kwa 3042 PARLIAMENTARY DEBATES August 8, 2007 kuileta Hoja hii. Ninasimama kuiunga mkono kama Mbunge. Sitaki kuingia katika masuala ya falsafa ya kibepari na kikomunisti, kwa sababu sioni kama ndio suluhisho la matatizo yanayowakumba wananchi na Wakenya kwa jumla. Lakini kuhusu masuala ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma, kwa sababu kama jina linavyoonyesha, ni mashirika yaliyopatikana kutokana na rasilimali za umma, ni muhimu kuwepo uwazi katika ubinafsishaji huo. Kwa nini nasema haya? Muda mchache uliopita, tuliambiwa kuwa Kenya Meat Commission (KMC) haiwezi kubinafsishwa kwa sababu itafilisika. Tuliangalia kwa muda wa miaka 15 na wafugaji hawakuwa na mahali pa kuuza mifugo wao. Leo imebinafsishwa, inaendelea vizuri, inaleta faida kwa nchi na mfugaji amepata suluhisho. Sasa ile fikra ya kusema kuwa utakapobinafsisha shirika la umma halitaleta faida si kweli. Kuna matatizo katika sekta ya utalii. Ndege inayowaleta watalii, gari linalowapokea wafikapo uwanjani mwa ndege na hoteli wanapokwenda kulala, vyote ni za wageni. Sasa ni vipi tutazungumza juu ya kupunguza umasikini katika nchi ya Kenya ilhali ndege mtalii anayosafiria gari linalombeba, hoteli anapokwenda kulala, na hata sehemu nyingine anazokwenda kuona katika nchi ya Kenya ni mali ya wageni? Vipi basi Mwafrika, au Mkenya, ataweza kupunguza umaskini katika nchi ya Kenya? Mbunge huyu anapoileta Hoja hii hapa, anatuuliza, kama Wabunge, tutekeleze wajibu wetu. Tuchunguze kindani ili mashirika haya yasipewe watu wachache bali yalete faida kwa Wakenya kwa jumla. Tutakapofikia masuala ya ubinafsishaji, iwapo Serikali imechoka kuendesha shughuli zake, kwa nini tusitoe hisa zake kwa Wakenya wazaliwa? Kama kuna mgeni ambaye anataka kumiliki hisa, anafaa kumiliki hisa hizo kupitia kwa Mkenya. Sina mengi; nimesimama kuiunga Hoja hii mkono."
}