GET /api/v0.1/hansard/entries/21033/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 21033,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/21033/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Jambo la Nidhamu, Bw. Spika. Mnamo 22/2/2011 niliuliza arifa kutoka kwa Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani kuhusu kuzorota kwa usalama katika Mji wa Eldoret na Mji wa Kitale. Tunajua mikahawa katika miji hii imekuwa ikivamiwa mara kwa mara na watu wengi kupoteza maisha yao kiholelaholela. Jambo la kuhuzunisha ni kuwa kufikia leo hakuna mshukiwa wowote ambaye amewahi kutiwa mbaroni na Waziri hajawahi kuleta arifa hapa Bungeni kutueleza vile mambo ya usalama yalivyo katika miji hiyo. Ninaomba Bunge hili kumzurutisha ailetee arifa hiyo kwa sababu kuzoroteka kwa usalama katika miji hiyo kumekita mizizi."
}