GET /api/v0.1/hansard/entries/211134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 211134,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/211134/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, ninasikitika kwamba hatuna muda wa kutosha kwa sababu ningependa kusema mengi kuhusu kwa nini hukumu ya kifo haihitajiki katika nchi hii. Kwanza, makosa hufanyika na watu ambao hawana hatia wameuawa. Wale ambao wanafikiria ya kwamba kwa sababu mtu amekufa aliyemuua lazima apewe hukumu ya kifo, wanaongea kama hawajui kwamba kuna aina zingine za adhabu ambazo zinaweza kuzuia uhalifu. Sio lazima mtu auawe ndio tuzuie uhalifu. Isitoshe, kama umemuua mtu, huwezi kumurekebisha tena. Ukikosea na umuue mtu ambaye hana hatia, hayo makosa hayawezi kurekebishwa. Huyo mtu atakuwa amekufa bure. Mimi mwenyewe nilikabiliwa na hukumu ya kifo mara mbili. Wakati mmoja nilishtakiwa na kesi ya uhaini kwa kutafuta uhuru huu wa pili. Kama ningeuawa, singekuwa hapa nikiongea. Labda huo uhuru wa pili ungekuwa vigumu kupatikana kama wote ambao walikuwa wanaupigania wangeuawa. Bw. Naibu Spika, pia nilishtakiwa kimakosa kabisa kwamba nilivamia kituo cha polisi na nikawekewa tena kesi ya hukumu ya kifo. Tunasema kuwa sisi ni wakristo katika nchi hii, lakini tunasahau ya kwamba kama sio hukumu ya kifo Yesu hangeuawa. Yesu aliuawa kwa sababu ya hukumu ya kifo kama hii ambayo Wakristo walio hapa wanaitetea. Kama hatungekuwa na hukumu ya kifo katika sheria zetu, labda hata sasa Dedan Kimathi angekuwa hai. Watu wengine wa kikundi cha Mau Mau waliouawa wakipigania Uhuru, walikufa kwa sababu ya hukumu ya kifo. Tuliletewa sheria hii na wakoloni na tukaichukua tuu. Bw. Naibu Spika, ukiangalia sheria za jadi, nyingi hazikuwa na hukumu ya kifo. Kulikuwa na kutoa ng'ombe au mbuzi lakini watu hawakuuawa. Jambo hilo lilikuwa nadra sana. Lazima tukumbuke maneno ya Mahatma Gandhi aliyesema kwamba: \"Tabia ya jicho kwa jicho itaacha taifa nzima likiwa pofu.\" Kwa hivyo, tusione kuwa kulipiza kisasi ni kufanya haki. Fikira kama hizi za kutaka kuua kwa sababu ya makosa ndizo zinasababisha washukiwa kuuawa na polisi hata kabla ya kupelekwa mahakamani. Watu wanakufa kwa wingi. Kama August 1, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2893 tungekuwa watu ambao wanaelewa kwamba sio lazima mtu auawe kwa makosa, hata wahukumiwa ambao wanauliwa wakati huu labda hawangekuwa wakiuawa. Kuna wale ambao wanasema mtu akiwa mhalifu lazima auawe hata kama hajafanyiwa kesi. Wengine wanasema mtu akiwa katika kundi la Mungiki lazima auawe. Hakuna sheria ambayo inasema kuwa mtu akiwa katika kundi la Mungiki au Taliban lazima auawe. Bw. Naibu Spika, ninaunga mkono Hoja hii na ninatumai kuwa hata Bw. Naibu Spika ataiunga mkono."
}