GET /api/v0.1/hansard/entries/211147/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 211147,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/211147/?format=api",
    "text_counter": 217,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Ndile",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Wildlife and Tourism",
    "speaker": {
        "id": 272,
        "legal_name": "Kalembe Richard Ndile",
        "slug": "kalembe-ndile"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, nasimama hapa kupinga hii Hoja. Nataka kumkumbusha rafiki yangu, Bw. Wamwere, kwamba Yesu asingalikufa, asingalisamehewa dhambi. Kwa hivyo, ulikuwa ni mpango wa Mungu kumleta mwanawe hapa afe ili tusamehewe dhambi. Nashukuru kwa sababu juzi nilimwona Agwambo akiombewa na wachungaji. Mtu akiamua kutenda maovu--- Najua kuna korti ambalo huchunguza kama aliua au la. Ikiwa aliua kwa bahati mbaya, korti lina uwezo wa kumsamehe, lakini inaweza kuwa alipanga, kama waliotaka kupindua Serikali na tukawapoteza watu wengi. Watoto wa vyuo vikuu walikufa, na hata watu wengine, ambao hawakuwa na hatia. Ni nani aliowaongoza? Hata juzi nilifikiri Agwambo angeombewa na hao wachungaji, kwanza asamehewe dhambi kwa sababu ya kuunga mkono jambo 2894 PARLIAMENTARY DEBATES August 1, 2007 hilo. Nilimwona akiombewa kule Kisumu, lakini badala ya kuombewa asamehewe dhambi, aliombewa eti awe rais. Nasema wangenyongwa kwa sababu ni lazima mtu akiamua kuuwa mwingine naye achukuliwe hatua. Tulipokuwa Bomas, Wakenya walikataa na wakasema kuwa hawawezi kumkubali mtu ambaye--- Kwa sababu mtu ataanza kuuwa na kusema: \"Hutanipeleka popote\"! Kwa hayo machache, siungi mkono."
}