GET /api/v0.1/hansard/entries/211399/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 211399,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/211399/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Mr. Moroto): Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili pia nitoe maoni kuhusu jambo lililo mbele yetu. Tunafahamu kwamba afya ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu na kiumbe chochote katika dunia. Kwanza, nataka kuishukuru Wizara ya Afya kwa kazi ambayo imefanya katika muda mfupi sana, tukielewa kwamba sehemu ambazo wengine wetu tunatoka zilikuwa zimesahaulika kwa muda mrefu sana. Pesa kidogo tunazopata kupitia CDF zimetusaidia kujenga vituo vya afya ili kuboresha maisha ya watu wetu. Jambo ambalo nauliza Wizara iangalie ni kwamba, ijapokuwa tumejenga vituo hivyo kupitia bidii ya wakaazi wa sehemu zetu, na kutokana na kitu kidogo kutoka CDF, hatuna madaktari. Najua kwamba wakati huu kuna wale ambao wataajiriwa na kuchukuliwa kwenda kusomea udaktari. Sehemu fulani, hasa zile kavu, nauliza Wizara ijaribu kuziangalia, ijapokuwa imepandisha sana gredi inayohitajika kuseomea udaktari. Ingefaa iteremshe gredi hiyo na kuangalia sehemu zilizoachwa nyuma kwa muda mrefu, ni vipi zitafaidika. Sisi kama Wakenya tuko pamoja. Wakati tulianza, tulianza pamoja lakini kuna wengi ambao wamepiga hatua zaidi ya wengine. Si kwamba wengine walipendelea kupiga hatua za polepole hivyo. Kuna wengine ambao walitunukiwa nafasi ya kuangalia kwamba usawa unapatikana, hawakufanya hivyo. Hii ndio sababu tunasikia kwamba kuna sehemu ambazo, hata sasa hivi, baada ya miaka zaidi ya 40 tangu tupate Uhuru, bado wanatumia mizizi ya miti kama dawa. Kwa sababu ya matumaini ambayo wananchi wanayo sasa, ningeuliza wale wanaohusika wajaribu kuona kwamba watu kama hao wamesaidia sawa na wengine. Nimezungumza kuhusu wale wanaokwenda kusomea udakitari, waliofuzu na ambao sasa wanaenda kuwatibu na kuwasaidia watu. Tunashuruku kwa kuwa Mhe. Rais alitembelea Kapenguria. Alipofika pale kuna sehemu ambayo ilikuwa imetengwa na wakaazi wa West Pokot hapo awali, na wakajenga mahali pa kuwafundishia vijana ambao wangeweza kufanya kazi ya utabibu; walijenga Medical Training College (MTC). Kuna jambo linalonisikitisha: imechukua muda, na hadi sasa hakuna hata kitu kinachoweza kuonyesha kwamba wale wanaohusika wanapanga kuwachukua wanafunzi na kuanza kufundisha katika chuo hiki. Kupitia runinga, tumeona ya kwamba kuna wachache ambao walijenga vyuo kama hivi vya Medical Training College (MTC) kupitia mradi wa kustawisha maeneo ya bunge wa Constituencies Development Fund (CDF). Sisi ni majirani na tunaweza kuwaona Wabunge wengine wanafanya nini. Ukisoma Kenya Gazette, utapata kwamba kuna wenye wamepewa nafasi ya kuchukua wanafunzi, kwenda kuwafundisha ili warudi kuwafanyia watu kazi. Lakini, wale ambao wanapewa jukumu hilo ni wale wanapeperusha bendera. Lazima Wizara itueleze: Ni lazima kila mtu awe na bendera ndio apewe jukumu hilo? Je, itakuwaje kwa wale ambao hawana bendera? Hilo ndilo jambo ambalo linatukera sana. Nauliza Wizara ione ya kwamba usaidizi unatolewa kwa haraka sana kwa watu wa Kapenguria. Ikiwa hakuna usaidizi, tuambiwe hakuna, ili tungoje wengine watakaokuja kutusaidia. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna vifaa ambavyo vinasaidia katika matibabu, kama X-Ray . Katika wilaya yangu, tuna hospitali ya wilaya moja ya Kapenguria. Ukichunguza katika kumbukumbu za miaka kumi iliyopita, hospitali hiyo haina X-Ray . Imebidi biashara zingine 2934 PARLIAMENTARY DEBATES August 1, 2007 kutokea kando. Mtu akiwa mgonjwa, analazimishwa kwenda kupata usaidizi kwa hospitali ya mtu binafsi. Jambo linalotushangaza ni kwamba X-Ray ya watu binafsi inawekwa karibu na hospitali. Wakati mgonjwa anahitaji usaidizi wa aina hiyo, anaambiwa: \"Enda kwa hiyo ya mtu binafsi!\" Serikali ina uwezo wa kuwasaidia watu wake. Naiihimiza Wizara ijaribu kuwasaidia wananchi wa sehemu hiyo, ili wasizidi kuumia jinsi wanavyoumia kwa wakati huu. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna mambo mengine ambayo Wizara imejaribu sana na namshukuru Waziri. Ugonjwa wa malaria umekuwa ukiumiza watu sana. Lakini Wizara imejaribu kupeana mosquito nets kwa shule na kwa akina mama waja wazito. Pongezi zetu zinaenda kwa Wizara kwa sababu tunaona ya kwamba maisha tuliyokuwa tukipoteza, kwa wakati huu, mambo hayo yamesahaulika. Kuna wakati mmoja tulitembelea mahali fulani na wazee wakongwe wakahesabu watato ambao wamepoteza kwa muda uliopita na wakafananisha na wale wanaoishi sasa. Walisema kwamba Mungu amewachukia. Ombi langu ni kwamba mambo machache ambayo yamebaki, kama vile vifaa vya hospitali kama X-Ray na shule ya MTC yatiliwe maanani. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine linahusu uchukuzi, yaani transportation . Kuna sehemu kavu sana katika nchi hii na utapata ya kwamba Wizara ya Afya inapeana gari kama"
}