GET /api/v0.1/hansard/entries/211403/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 211403,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/211403/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwaboza",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Immigration and Registration of Persons",
"speaker": {
"id": 243,
"legal_name": "Anania Mwasambu Mwaboza",
"slug": "anania-mwaboza"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii kuhusu Bajeti ya Wizara ya Afya. Tunavyojua, afya ni utajiri. Ikiwa afya ni utajiri, basi utajiri huu u namna gani? Katika mipangilio ya huduma za afya katika nchi--- Nafikiri baada ya kupigania Uhuru, swala la kwanza lilikuwa kuhakikisha kwamba Mwafrika amejikomboa kutoka kwa magonjwa ili watu wapate huduma za tiba bora. Imekuwa aje kwamba miaka 43 baada ya Uhuru, katika sehemu zingine na mikoa mingine katika nchi hii, bado wananchi wanalia kuhusu maswala ya tiba? Kwa mfano, katika hospitali za mikoa--- Kwa mfano, hivi majuzi, huduma ya maji ilikatwa katika Hospitali ya Mkoa wa Bonde la Ufa. Tunajua kwamba katika hospitali, bila huduma ya maji, basi mambo mengi hayawezi kufanyika. Katika Hospitali ya Mkoa wa Pwani, mambo ni vile vile na huduma ya maji ilikatwa. Mambo kama upigaji picha za eksirei hazipo. Wananchi wanalazimika kwenda katika huduma za afya za kibinafsi ambapo wanalipishwa mara tano ile fedha wangelipa katika hospitali za Serikali. Mambo mengine kama vile viwango vya wazazi wanaozaa na watoto wanaofariki, ambayo Waingereza wanaiita infant mortalityrate, imeongezeka hata katika hospitali za mikoa. Hivi majuzi, katika hospitali ya Mkoa wa Pwani, watoto sita walipoteza maisha yao kwa sababu ya kifaa fulani ambacho hakikuwepo na gharama yake ni Kshs1.5 million. Jambo kama hilo linawezekana aje?"
}