GET /api/v0.1/hansard/entries/212065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 212065,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/212065/?format=api",
    "text_counter": 230,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kuniona na kunipa nafasi niunge mkono Hoja hii kwa dhati sana. Kwa sababu sina wakati wa kutosha, nitasema kwa mukhtasari. Mawazo yote ambayo yamesemwa na Waziri Msaidizi hapa ni yale ya kuitazama nchi kupitia mfumo wa ubepari. Tunajua sekta ya binafsi inapata faida sana kutoka na kuimarika kwa uchumi. Ingawa uchumi wetu unakuwa kwa haraka sana lakini nafasi za kazi haziongezeki. Sekta ya umma au ya Serikali ina jukumu la kuwapa wananchi wake nafasi za kazi. Kwa hivyo, Hoja hii ambayo inasinikiza sekta ya Serikali iajiri walimu, waguuzi na wanafanya kazi wengi katika idara mbalimbali za Serikali na pia kuhimiza sekta ya binafsi kufanya hivyo, ni Hoja ya maana kabisa. Kwa hivyo, naomba Bunge hili kwa mukhstari kuunga mkono Hoja hii. Ni Hoja ya maana sana na itatusaidia kutengeneza nafasi nyingi za kazi."
}