GET /api/v0.1/hansard/entries/212069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 212069,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/212069/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Mr. Kingi); Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili niunge mkono Hoja hii. Hoja hii ni muhimu sana katika maisha yetu sisi kama Wakenya. Ninakubaliana kabisa ya kwamba sekta ya umma ni lazima iwe na sera maalum ya kuhakikisha ya kwamba wananchi au Wakenya wanaajiriwa. 30 PARLIAMENTARY DEBATES July 25, 2007 Bw. Naibu Spika wa Muda, kila siku hapa tunajibu maswali kuhusu usalama wa taifa hili. Tatizo kubwa tulionalo ni kwamba askari wetu ni wachache na hawatoshi. Kiwango cha askari tulionayo ni kama askari mmoja anachunga wananchi 1,000. Kwa hivyo, tunataka Hoja hii ipitishwe ili Serikali iweze kuwaajiri askari wengi watakaoweza kuimarisha usalama wa taifa hili."
}