GET /api/v0.1/hansard/entries/212071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 212071,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/212071/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ukiangalia matatizo tuliyonayo katika shule zetu, utaona kwamba tunapeana masomo bila malipo. Lakini ni walimu wangapi wako katika shlule hizo kuhakikisha kwamba watoto wetu wanapata elimu bora? Tuna walimu wachache sana. Kwa hivyo, Hoja hii ikipitishwa, tutahakikisha kwamba kuna wafanyikazi wa kutosha katika shule zetu na hospitali ambazo ziko kwa wakati huu na zile ambazo tunaendelea kujenga. Baada ya hayo, tunaweza kuangalia mambo ya sekta ya kibinafsi. Ni lazima Serikali ichukue jukumu hili na kuhakikisha kwamba wananchi wanahudumiwa kwa njia inayofaa."
}