GET /api/v0.1/hansard/entries/212075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 212075,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/212075/?format=api",
    "text_counter": 240,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii kwa sababu nchi hii ina haja kubwa ya kuzalisha kazi ili tuweze kumaliza uhalifu. Kuna watu wengi ambao wanaamini kwamba njia bora ya kumaliza uhalifu ni kuua kila asiyekuwa na kazi. Lakini ukiniuliza, dawa ya kumaliza uhalifu ni kuwapa vijana kazi. Tukiwapa kazi hatutakuwa na vikundi kama vile Mungiki, Sabaot Defence Force au Mombasa Republican Council. Hakuna njia nyingine. Tuwapatie vijana kazi kwa kutumia mbinu hii ambayo ilitumiwa Marekani na ikafaulu. Tunahitaji kuwatumia vijana kujenga mabwawa, barabara na tuwapatie mashamba. Nchi hii ina mashamba mengi ambayo hayatumiwi. Wale ambao hawayatumii mashamba yao ndio wanababaika kwamba Hoja kama hii itakuja kuwalazimisha kupeana mashamba yao kwa wale ambao hawana kazi ili nao waweze kuishi. Bw. Naibu Spika wa Muda, kama Serikali, tunasema ya kwamba tumefanya zaidi ya yale yanayoulizwa na Hoja. Kama mtu amekuuliza umpe vitu tano na umempa kumi, kwa nini unapinga Hoja hii? Kwa hivyo, kama Serikali, tumefanya zaidi ya haya na hiyo ndiyo sababu tunaunga mkono Hoja hii. Hatuwezi tukapinga Hoja hii na tukarudi hapa Bungeni. Tutatupwa nje na wananchi. Ni lazima tuelewe siasa. Siasa ni kuwasaidia watu wale hawana kazi wala si kuwapinga wale wanalilia kazi. Hata sielewi ni kwa nini Waziri Msaidizi alikuja kusoma taarifa yake. Naona ni kitu aliandikiwa na akaja kusoma bila ya kuunga mkono. Hata sauti yake ilisikika hivyo!"
}