GET /api/v0.1/hansard/entries/212296/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 212296,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/212296/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Awori",
"speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
"speaker": {
"id": 290,
"legal_name": "Moody Arthur Awori",
"slug": "moody-awori"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili nami nichangie machache kuhusu kazi ya Wizara hii. Nafikiri sitakuwa nikimaliza wakati wa Bunge hili nikiwakumbusha Wabunge kwamba barabara ni muhimu kwa uchumi wa nchi. Ikiwa barabara zimeharibika na kuzoroteka, ni shida kusafirisha nafaka kutoka kwa stoo au mashambani hadi mahali pa kuuza. Hiyo itafanya uchumi uende chini. Kwa kweli, kwa miaka hiyo iliyopita, tumeona kwamba barabara zetu zilikuwa zimezoroteka sana. July 25, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2777 Ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza sana Waziri na maofisa katika Wizara yake kwa kazi njema wanayofanya. Siku hizi, harakati za marekebisho ya barabara zinaonekana. Kokote unakokwenda katika nchi hii utakuta mashine zikifanya kazi. Zamani, ilikuwa ni katika maeneo yale yaliyosemekana kuwa \"politically-correct\" ndiko ungekuta mashine ya kujenga barabara. Wakati huu, ni katika sehemu zote za nchi ambako utakuta watu wakifanya kazi. Jambo la kusikitisha ni kwamba mara nyingi hatuwezi kutumia hizo pesa zote. Hii ni kwa sababu ya upungufu wa nguvu tunazoweza kutumia kufanya kazi. Hii imetokana na uhaba wa wahandisi jinsi Waziri mwenyewe alitueleza hivi majuzi. Watoto wetu wengi waliohitimu kuwa wahandisi wamehama nchi hii na kuenda nchi nyingine."
}