HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 212298,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/212298/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Awori",
"speaker_title": "The Vice-President and Minister for Home Affairs",
"speaker": {
"id": 290,
"legal_name": "Moody Arthur Awori",
"slug": "moody-awori"
},
"content": "Ukienda Botswana, utaona kwamba wahandisi wakubwa wametoka nchini Kenya. Vile vile, tuna uhaba wa wanakandarasi wenye uwezo wa kuchukua kandarasi kubwa. Sisi kama Serikali, sasa tunataka kuweka mazingira bora ambayo yatawashawishi vijana wetu waliohamia nchi za nje waregee nchini ili wachukue jukumu la kutusaidia kurekebisha barabara zetu na kujenga barabara nyingine. Tunataka kuongeza harakati za kurekebisha barabara. Kuna maafa mengi sana yanayosababishwa na ajali zinazotokea barabarani kwa sababu hatujaweza kuwa na uwezo wa kuifanya hiyo kazi kwa upesi. Lakini sisi ni lazima tuipongeze Wizara wakati huu. Tumeona kwamba kazi inaendelea vizuri. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna mambo machache ambayo ningependa kumshawishi Waziri na wahudumu wake wayatilie mkazo. Mara kwa mara, pesa zinatengwa ili tuweze kuweka maramu katika barabara fulani. Kuna sehemu ambako tumetumia kama Kshs90 million, lakini kunaponyesha punde tu kazi hiyo inapokamilika, barabara yote inaharibika. Wakati umewadia sasa wa kutafakari juu ya jambo hili. Labda, inafaa tuache kuharibu pesa nyingi sana tukiweka maramu barabarani na badala yake tuwe tunazifanyia barabara hizo grading tu, na zile pesa ambazo zinazosalia zitumiwe kuweka lami. Ningependa kuitoa kama mfano Barabara C30, ambayo kwa miaka mingi sana, kila mwaka, ilitengewa zaidi ya Kshs100 milion na kabla ya mwaka kuisha, kunaponyesha, barabara hiyo inaharibika. Ilichukua zaidi ya miaka 15. Ukipiga hesabu, utaona kwamba Kshs1.5 billion zilitumiwa lakini hatukufua dafu. Sasa barabara hiyo imeanza kuwekwa lami. Ninajua kwamba kandarasi hiyo imegharimu chini ya Kshs1 billion. Ningependa tufikirie sana jinsi tutakavyo hifadhi pesa kidogo kidogo ili tukiwa na barabara ya kuweka lami, tuanze tu kuiweka lami. Hazina kama hiyo inaweza kutusaidia. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kutoa shukurani kwa Waziri na wahudumu wake kwa kuanzisha mpango wa kuiweka lami barabara hiyo, ambayo mimi huitumia sana. Sasa tunataka kuona kwamba iwapo mwanakandarasi anafanya kazi vyema, stakabadhi zake za malipo zinapotayarishwa, awe analipwa upesi. Vile vile, ningependa kuomba kwamba barabara inapowekwa lami, barabara hiyo ikipitia sokoni, au karibu na makao ya tarafa, kutengwe pesa nyingine kidogo ambazo huyo mwanakandarasi atatumia kuiweka lami barabara inayoingia kwenye soko hilo. Barabara kama hiyo inaweza kutusaidia. Ningependa kumuomba Waziri kwamba, kama inawezekana, kwa vile mwanakandarasi anayeiweka lami katika barabara hiyo bado yuko katika sehemu za kwetu, ikubaliwe ili mwanakandarasi huyo aweke lami barabara zinazoingia kwenya Masoko ya Funyula na Port Victoria, miongoni mwa mengine, pamoja na barabara inayoelekea kwenye ofisi ya DO. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuhusu suala la kuhifadhi barabara, miaka mingi iliyopita 2778 PARLIAMENTARY DEBATES July 25, 2007 kandokando ya barabara kulikuweko na kambi za wahudumu ambao walikuwa wakihifadhi na kurekebisha barabara. Utaratibu huo uliwawezesha wahudumu hao kurekebisha kwa haraka sehemu za barabara zilizohitaji kurekebishwa. Kulikuweko na inspectors ambao walikuwa wakizikagua barabara mara kwa mara. Kambi hizo zikirudishwa hivi sasa, mashimo yanapotokea kwenye barabara zetu za lami, yataweza kuzibwa kabla ya kuwa makubwa zaidi. Tumelizungumzia sana suala la kuzisimamia barabara zetu kwa msingi wa kibiashara. Wakati sasa umewadia wa kuwatafuta wawekezaji wazichukue na kuzisimamia barabara zetu kubwa kupitia mpango wa kuwatoza wenye magari pesa kidogo ili tuweze kurekebisha barabara zote humu nchini. Pia, tunataka Wizara iwasiliane na National Environment Management Authority (NEMA), ambayo inashughulikia maswala ya mazingira humu nchini. Litakuwa jambo la busara iwapo kutakuweko na sharti, katika stakabadhi za tenda, litakalomlazimu mwanakandarasi kupanda miti kandokando ya barabara atakayojenga. Sharti hilo litatuwezesha kuwa na miti mingi sana humu nchini. Bw. Naibu Spika wa Muda, katika miji mikubwa kama Nairobi kuna msongamano mkubwa sana wa motokaa. Tunataka kuuangalia mpangilio wa barabara zetu ili tuona kama tunaweza kujenga milingoti, halafu juu yake tuweze kujenga barabara. Kuna miji mingi mikubwa kama ile ya Malaysia, Korea, na kwingineko, ambako serikali zimefanya hivyo. Kufanya hivyo kunasaidia kupunguza msongamano wa motokaa. Ningependa kumwomba Waziri aanze kulifikiria jambo hilo. Nikizungumza kuhusu District Works Committees, ninazipongeza, lakini, wakati sasa umefika wa kuziongezea ruzuku kamati hizo katika kila sehemu ya uwakilishi Bungeni kwa kiasi cha kati ya Kshs15 million na Kshs20 million ili tuweze kukamilisha kutengeneza barabara ndogo ndogo. Mwisho, ni ombi tu kwa Wizara kwamba kuna watu wengi wanaotaka kusafiri kwa ndege hadi makwao, au kwingineko, ili waweze kuhifadhi masaa ya kufanya kazi. Tungependa Wizara izingatie suala la kuvirekebisha viwanja vidogo vidogo vya ndege. Kuna airstrip ambazo hazikuwa zikishughulikiwa kwa muda mrefu, na ambazo zimeharibika. Airstrip hizo zinahitaji kurekebishwa, na nyingine mpya zianze kujengwa. Ingekuwa bora kama Wizara ingeanza na"
}