HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 212321,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/212321/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Karume",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 234,
"legal_name": "Njenga Karume",
"slug": "njenga-karume"
},
"content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ninasimama hapa kuunga mkono bajeti ya Wizara ya Barabara na Ujenzi kwa sababu wanafanya kazi ya maana sana nchini. Ninataka pia kumshukuru sana Waziri kwa kazi yake nzuri. Tunajua hajamaliza miaka miwili katika Wizara hii lakini amefanya mambo mengi. Ukitazama kila eneo Bunge na wilaya, utaona ya kwamba kuna ujenzi au ukarabati wa barabara. Hapo awali, barabara zetu hapa nchini zilikuwa zimeharibika kabisa. Barabara zetu, hasa Wilaya ya Kiambu, zilikuwa zimeharabika sana kiwango cha sisi kuweka kokoto na changarau ili magari yetu hasikwame. Wakati huu, Wizara hii inafanya kazi ya maana sana katika pembe zote za 2784 PARLIAMENTARY DEBATES July 25, 2007 nchi hii bila kubagua sehemu au watu fulani. Bw. Naibu Spika, mwaka jana tulikuwa na mvua kubwa hapa nchini. Mvua hiyo iliharibu barabara nyingi hapa nchi. Mkoa wa Pwani uliathirika sana; daraja nyingi ziliharibiwa. Lakini maofisa wa Wizara hii walifanya kazi usiku na mchana ili kuzirekebisha. Ninawashukuru wafanyakazi wote wa Wizara hii kwa kazi yao nzuri ya kurekebisha barabara zetu. Hata watu wa Mkoa wa Pwani hawangeweza kusafiri hadi Tanzania kwa sababu ya kuharibika kwa barabara. Kwa sababu ya juhudi zao, kwa muda mfupi waliweza kurekebisha barabara hizo na mambo ya biashara yakaendelea sawasawa. Kwa hivyo, tukiwapa pesa nyingi wataweza kufanya kazi nzuri sana hapa nchini. Pesa hizi ambazo tunahitajika kuzipitisha leo, haziwatoshi. Serikali inafikiria sana kuimarisha barabara za nchi hii. Ninaiomba Serikali ifikirie kuiongezea Wizara hii pesa nyingi ili ifanye kazi nzuri zaidi hapa nchini. Juzi, Waziri alizungumza juu ya kandarasi za barabara. Alisema wajenzi wa barabara fulani wanafanya kazi yao polepole sana. Ningependa kuona wanajitahidi sana ili wafanye kazi kwa haraka. Ikiwa kuna wajenzi ambao hawamalizi kutengeza barabara kwa muda fulani, basi wasilipwe pesa hata wakifanya kwa muda zaidi. Hawa ndio wanaotakiwa kukazwa kwa sababu hatujui kwa nini wanafanya kazi yao polepole. Kwa hivyo, watu wamefurahia sana kazi ya Wizara hii. Hii inaonyesha ya kwamba Serikali yetu inayoongozwa na mhe. Mwai Kibaki inafanya kazi nzuri. Si ukarabati wa barabara pekee, bali inafanya kazi katika sehemu zote za nchi. Barabara zinawekwa lami kila mahali. Kamati za Barabara za Wilaya pia zinafanya kazi ya maana sana. Lakini taabu ni vile barabara hizi zilikuwa zimeharibika kwa muda mrefu. Kwa hivyo, kuzirekebisha, kutachukua muda. Ni wazi kwamba Wizara hii ikipata pesa za kutosha itaweza kufanya kazi ya maana sana. Inafaa kamati hizi zipewe pesa nyingi ili wakarabati barabara huko mashinani. Bila kuwa na barabara za kutosha hata mambo ya biashara yataathiriwa. Sekta ya ukulima ni ya maana sana katika nchi yetu. Hata wakulima wakifanya kazi bidii, bila barabara nzuri, hawataweza kuuza mazao yao. Bw. Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu utalii. Watalii wanailetea nchi hii pesa nyingi sana. Tunakumbuka hapo awali, utalii ulikuwa umeathiriwa sana nchini. Watalii wengi hawangetembelea nchi yetu kwa sababu ya barabara mbaya. Lakini vile Wizara hii inatengeneza barabara, hasa upande wa Pwani, watalii wameanza kuja kwa wingi. Kwa hivyo, ningependa kumhimiza Waziri aendelee kufanya kazi hiyo nzuri. Bw. Naibu Spika, katika Kiambaa na Wilaya ya Kiambu kwa jumla, barabara za lami zilikuwa zimekwisha. Magari yalikuwa yanakwama huko lakini furaha ni kwamba Wizara imeanza kuzitengeneza barabara hizo. Kwa hivyo, inafaa Wizara hii ipewe pesa za kutosha ili iendelee kufanya kazi nzuri. Pesa hazijatosha lakini najua wakipatiwa pesa, watatengeneza barabara zetu. Bw. Naibu Spika, naungana na Wabunge wengine kufikiria vile hii Wizara inaweza kusaidiwa zaidi katika ujenzi wa barabara. Waziri anajua Kiambaa sana na mimi sitaki kumwambia huko kuko namna gani. Sote wawili tunajua vile ameanza kututengenezea barabara ya kutoka Gachie hadi Kanyungu. Najua ujenzi wa barabara hiyo utakamilika haraka. Hiyo barabara ilikuwa imeharibika kabisa kiasi kwamba hata usiku wagonjwa hawangefikishwa katika hospitali. Kuna hospitali ya maana sana hapo. Wakati hospitali za karibu ziko na dawa, hiyo inasaidia kwa sababu badala ya wagonjwa kwenda Kenyatta National Hospital (KNH) wao wataenda katika hospitali zilizo karibu nao. Kwa hivyo, mimi nashukuru kwa hiyo barabara ambayo imeanza kutengenezwa. Najua kuwa zile barabara nyingine, kwa mfano, ile ya Ndumberi-Kanunga-Banana- Ndenderu itatengenezwa. Hii barabara ndiyo nilisema kwamba zamani ilikuwa ya lami lakini hiyo lami ikakwisha. Najua pia wanakumbuka barabara ya Ndumberi-Limuru-Githiga. Furaha yangu ni kujua kwamba sasa kuna watu katika Wizara ambao tunaweza kwenda kuwaona ili tuwaambie shida zilizoko kwenye barabara zetu. Hata Waziri atakuja kuziona barabara hizo mwenyewe. Wafanyikazi wote wa Wizara hii wako imara sana na kwa hivyo najua kwa kweli hii kazi ya July 25, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2785 barabara itafanywa. Ningependa kuiuliza Serikali ikipata pesa nyingi hata kabla ya Bajeti ya mwaka ujao, ijaribu kusaidia Wizara hii ya barabara ndiposa iweze kutengeneza barabara nyingi zaidi. Bw. Naibu Spika, najua kuna Wabunge wengi sana ambao wangetaka kuzungumza kuhusu mambo ya barabara. Nitakomea hapo. Ahsante sana na naiunga mkono Hoja hii."
}