GET /api/v0.1/hansard/entries/213116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 213116,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213116/?format=api",
    "text_counter": 196,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja juu ya kuwatakia polisi masilahi na mishahara bora zaidi. Nadhani hili ni jambo ambalo haliwezi kupingwa na yeyote kwa sababu maofisa wa polisi, kama vile Wakenya wengine, wanahitaji mishahara na nyumba bora za kuishi. Zile nyumba wanamokaa zinazoitwa A-frame structure ni vyumba ambavyo havistahili kuwepo tena. Bw. Naibu Spika wa Muda, nakumbuka zamani sana tukibishana na Mkuu wa Polisi katika Mkoa wa Bonde la Ufa, Bw. Mbijiwe. Wakati nilisema polisi wanastahili kujengewa nyumba bora zaidi, niliporudi nyumbani nilikutana naye na akawa mkali sana kwangu akisema sina haki ya kuwatetea maofisa wa polisi. Nadhani ni kwa sababu ya upinzani wa aina hiyo kutoka ndani ya polisi yenyewe ya kwamba maofisa hawa wameendelea kuishi katika nyumba ambazo hazistahili binadamu kuishi. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia swala la bima ni muhimu kwa polisi ambao wanakufa wakiwa kazini. Familia zao zina haki ya kushughulikiwa au kuhakikisha ya kwamba zinaishi katika hali inayostahili baada ya kufiwa na bwana na hata mabibi zao. Ili polisi wetu waweze kufanya kazi yao wanavyostahili ni muhimu---"
}