GET /api/v0.1/hansard/entries/213119/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 213119,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213119/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nilikuwa nasema ni muhimu wakumbushwe kutekeleza kazi yao kwa usawa kwa sababu nadhani bado kuna tatizo miongoni mwa polisi. Kuna tatizo la kusema ya kwamba polisi wanatekeleza ule wito wao wa utumishi kwa wote bila ubaguzi. Wakati mwingine unakuta ya kwamba polisi wakihitajika kwenda kuwahudumia matajiri, wao huenda haraka kuliko wakati wanahitajika kuwahudumia maskini. Hili nalijua kwa sababu wakati mwingine hata utakuta kuna matajiri au viongozi wanafanya uhalifu ambao unaonekana hata katika runinga lakini unakuta hawashtakiwi. Je, kuna sheria mbili; moja ya viongozi na matajiri na nyingine ya maskini? 2584 PARLIAMENTARY DEBATES July 18, 2007 Masikini akionekana akimpiga mwenzake ngumi vile Kimani Ngunjiri alivyoonekana akimpiga wakili mmoja kule Nakuru, analala ndani. Watu walioufanya ushenzi huo bado wanatembea na bado wako huru. Tunashindwa kuelewa sheria hii inatakiwa kufuatwa na nani. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna swala lingine nyeti ambalo limenisumbua kwa muda mrefu. Tumepitisha sheria ya kuwalinda wapiga firimbi lakini utakuta kwamba wapiga firimbi wanapotoa habari kuhusi ufisadi unaohusu watu kama Kamlesh Pattni wanaomiliki hoteli kubwa kama ile ya Grand Regency, hata baada ya mahakama kusema kwamba ni haki ya wapiga firimbi kurudishwa katika kazi walizofutwa, wanashindwa kurudi kazini. Wanapoenda huko hotelini, wanakuta kwamba majambazi wameajiriwa kuhakikisha kwamba hawarudi kazini. Watu hao wamezunguka kwa zaidi ya miaka karibu mitano na hawana pa kwenda. Pia wameenda katika Wizara na Ofisi ya Rais, ambayo inasimamia polisi wote. Vile vile, wameenda katika Wizara ya Haki na Katiba ambapo huwa wanapewa barua za kuonyesha kwamba wana haki ya kurudi kazini, lakini sasa umefika wakati ambapo hawajui watakwenda kwa nani."
}