GET /api/v0.1/hansard/entries/213417/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 213417,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213417/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kingi",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
    "speaker": {
        "id": 248,
        "legal_name": "Joseph Kahindi Kingi",
        "slug": "joseph-kingi"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii ambayo nimepatiwa. Yangu yatakuwa machache. Kwanza, ningependa kuipongeza Wizara ya Elimu kwa jinsi inavyoendesha shughuli zake kuanzia wakati Waziri, pamoja na wenzake, walipopewa usukani wa kuiendesha Wizara hii. Ninawapongeza haswa kwa vile Wizara hii iliichukulia ile shughuli ya nyongeza ya mishahara ya waalimu, ambayo ilikuwa imeleta matatizo mengi kwa taifa hili katika miaka michache iliyopita. Ningependa kusisitiza kwamba kila wakati kunapokuwa na matatizo, inafaa kuwe na mawasiliano kati ya waalimu na mwajiri wao, kwa sababu mawasiliano \"huzaa\" mapatano na kuondoa mapambano. Bw. Naibu Spika wa Muda, pia ningependa kuzungumza kuhusu shule za kibinafsi, ambazo zimejitokeza kila mahali nchini. Ukitembelea sehemu yoyote humu nchini, utaona kwamba kuna shule za kibinafsi. Nyingi za shule hizo hazina vifaa vinavyohitajika. Shule hizo hazina viwanja vya kutosha, madarasa, hata madawati. Nyakati nyingi, shule hizo huwa hazina waalimu wa kutosheleza mahitaji ya wanafunzi wote, lakini unapata zinaendeshwa tu kinyume cha sheria. Ningependa kuiomba Wizara iwatumie maafisa walioko, pamoja na mawasiliano mazuri 2634 PARLIAMENTARY DEBATES July 18, 2007 katika Utawala wa Mikoa, ili tuhakikishe kwamba tumeacha tu zile shule za kibinafsi ambazo zinaweza kuyakidhi kikamilifu maslahi ya wanafunzi. Ningependa kuona kwamba zile shule za kibinafsi ambazo hazina vifaa vya kutosha zimefungwa na wanafunzi kutoka shule hizo wamehamishiwa kwingineko. Pia, ningependa kuzungumzia swala la kuwapandisha vyeo waalimu. Kuna waalimu wengi ambao mpaka sasa bado hawajapandishwa vyeo licha ya kwamba wamefanya kazi katika kiwango kimoja kwa miaka mingi. Kwa wale wachache ambao wamesalia, inafaa Serikali ifanye mpango wa haraka ili waweze kupandishwa vyeo, ndiyo wapate motisha ya kuifanya kazi hiyo ya ualimu kwa bidii zaidi. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}