GET /api/v0.1/hansard/entries/213713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 213713,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213713/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Capt. Nakitare",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ninauliza juu ya mambo ambayo yametendeka katika Saboti Constituency, ambayo inahusu nchi mbili, usiku wa 15 Jumapili, 2007 jioni. Majangili ambao hawajulikani waliuwa watu zaidi ya kumi na wakamchinja mwalimu ambaye ni makamu wa mwalimu mkuu wa shule yetu ambaye ni mke wa diwani Wasike katika Saboti Constituency. Ilichukua muda wa masaa tisa; kutoka saa tatu jioni mpaka karibu saa kumi na mbili asubuhi, ndipo walinzi wa usalama, akiwemo Mkuu wa Wilaya, walipoenda kushuhudia hayo mauaji. Bw. Naibu Spika, ninaomba Waziri atueleze, kwa sababu hili ni lengo la kabila moja. Juzi kulikuwa na mauaji Kinyoro ya watu 11. Kukawa na mauaji mengine Matisi ya watu 12. Hiki ni kielelezo cha kusema kwamba huo mwenendo wa mwaka wa 1992 umerudi kwa lengo la kumaliza kabila moja."
}