GET /api/v0.1/hansard/entries/213770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 213770,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213770/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": " Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mwenyezi Mungu anatuambia:- \"Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba mwanadamu kwa pande la damu. Soma, Mola wako ni mtukufu mno ambaye amemfunza kuandika kwa kalamu. Amemfunza mwanadamu asilolijua.\" Bw. Naibu Spika wa Muda, hayo si maneno yangu bali ni maneno yake Mwenyezi Mungu katika Kurani tukufu Sura 96, Aya ya kwanza hadi ya tano. Kuhusu umuhimu wa elimu, Mwenyezi Mungu ametoa mfano huu kuthibitisha kufaulu kwa mwanadamu humu duniani na ahera keshoye. Ili mwanadamu apate kutatua matatizo yake, inategemea ni elimu aina gani mwanadamu amefunzwa. Mbali na hayo, ninasimama kuunga mkono Hoja hii. Siyo kwa sababu niko upande wa kulia wa Bunge hili bali ni kwa sababu nilivukia upande wa kulia wa Bunge hili kwa minajili ya elimu bora inayotolewa kwa watoto wa nchi hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa uchumi unaokuwa kama wa Kenya, kutenga Kshs115 bilioni kwa ajili ya elimu ni swala ambalo halifai kusahaulika licha ya changamoto za kisiasa zilizopo. Wengi watajigamba leo eti watapeana elimu ya bure ya shule za upili. Mimi ninashangazwa kwa sababu wengine wao waliwahi kuwa Mawaziri katika Wizara ya Elimu lakini nasikitika kwamba hawakuwahi kuota ndoto hiyo walipokuwa Mawaziri. Leo ni rahisi wao kuwadanganya Wakenya eti watapeana elimu ya bure kwa shule zote za upili."
}