HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 213772,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213772/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wario",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda nitaliondoa neno hili na badala yake niseme watapotosha Wakenya kwa sababu wanaota ndoto isiyotekelezeka. Leo, elimu ya bure imetolewa kwa watoto. Watoto wafugaji wasiokuwa na tamaa ya kufika Darasa la Nane, leo wameacha kuchunga mifugo na kila mmoja anakimbia kuelekea July 17, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2547 darasani kung'ang'ana kama watoto wengine wa Kenya. Serikali, kupitia tuition, imesema kwamba karo inayotolewa kwa ajili ya masomo itaondolewa mwaka ujao. Huo ni mzigo wa pili wa Mkenya kuondolewa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni vigumu mtu kuamka siku moja kujenga nyumba na kuikamilisha. Hii elimu ya bure ina matatizo mengi. Kuna ukosefu wa karakana na shida za uajiri. Maswala haya siyo ya kuamka siku moja na kuyatekeleza. Hivyo, basi, elimu bila malipo ni nyota inayong'ara katika Bara la Afrika. Imekuwa jina na picha nzuri ya Serikali hii. Hivyo, basi, mimi nachukuwa fursa hii kumshukuru Waziri, Wizara ya Elimu pamoja na Serikali kwa kuleta fikira hii na kuendeleza mazungumzo hayo. Leo, masomo katika shule za msingi ni ya bure kwa watoto wetu. Pia, tuna ndoto kwamba matatizo makubwa yanayokabili shule za upili huenda yakatatuliwa hivi karibuni. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kuomba Wizara na vile vile niwakumbushe mambo kuhusu mtoto mfugaji. Kwa nini ninawakumbusha? Ukisoma Ripoti ya Ominde ya 1973 na ile ya Koech ya 1997, ikiwa sikusahau, zimegusia maswala ya wanafunzi kujiandikisha shuleni. Baada ya kuileta sera ya elimu ya bure, maswala yale yaliondolewa. Hata hivyo, tunakotoka sisi wengine, hasa nikuzungumza kuhusu sehemu kame za nchi hii---Tutakapozungumza juu ya idadi ya walimu na mpangilio wa masomo kwa watoto wanaotoka katika jamii za wafugaji, nafikiri kwamba huenda itakuwa ndiyo chanzo cha watoto hao kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa. Ningependa kutoa mfano wa Wilaya ya Tana River. Wilaya hii, zaidi ya miaka 25 iliyopita, imekuwa \"ikiongoza kwa nyuma\". Inajulikana wazi kwamba katika mitihani ya kitaifa ya Kenya, Wilaya ya Tana River huwa mwisho. Kwa muda wa nusu karne sasa, Wilaya ya Tana River imeshikilia nafasi hiyo ya mwisho. Je, wale walio katika Idara ya Uhakiki wa Ubora na Viwango, yaani Directorate of Quality Assurance and Standards wamefikiria nini kuhusu swala hili? Je, Wizara inapaswa kuleta mikakati ya aina gani? Hii ni kwa sababu wilaya moja \"kuongoza\" kutoka nyuma kwa miaka 25 ni swala ambalo lazima tujiulize kama taifa. Ni lazima tujue pengo liko wapi, matatizo ni gani na ni vipi tunastahili kusuluhisha shida hiyo. Aidha, ni muhimu tuelewe ikiwa ni muhimu kumfanya mwanafunzi kutoka jamii ya wafugaji kushindana na watoto wengine wa nchi hii. Kwa hivyo, ninawakumbusha kwamba hilo ni ombi tu. Ninaishukuru Wizara kwa kutenga pesa kwa minajili ya utoaji wa maziwa na chakula shuleni. Katika sehemu nyingi humu nchini, kuweko na hakikisho la kupata chakula ni tatizo kubwa. Utaona kwamba pasipokuweko na maziwa na chakula, idadi kubwa ya watoto hawataweza kwenda shuleni. Kwa hivyo, ninatoa shukurani yangu na kuipongeza Wizara kwa kuhakikisha kwamba maziwa na chakula vinatolewa kwa watoto shuleni, haswa katika shule za msingi. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunazungumza juu ya shule za msingi, lakini kuna \"shule za msingi\" zaidi kuliko zile shule za msingi tunazozungumzia. Ningependa kuiomba Wizara ifikirie jinsi itakavyoshughulikia shule za kiwango chini ya zile za msingi kwa sababu wengi wa watoto katika shule hizo wanasomeshwa kupitia michango ya wanavijiji. Wakati mwingine senti hupatikana na wakati mwingine hukosekana. Hali hii inaharibu motisha ya wale wanaofundisha watoto ambao bado hawajafikia kiwango cha shule ya msingi. Tukizungumza juu ya bursary, motisha kwa waalimu, kuboreshwa kwa karakana, na kila kitu ambacho ningegusia leo tunaona kwamba kimetengewa hela katika Bajeti. Mishahara ya waalimu imeongezwa. Kuongezeka kwa motisha ya waalimu kutaongeza motisha ya watoto wetu. Kuhusu uboreshaji wa karakana, nikichukua mfano katika sehemu ninayowakilisha Bungeni, tumejenga madarasa zaidi ya 100 kwa muda wa miaka minne. Tulifanya hivyo kwa ushirikiano wa hazina ya CDF na Wizara ya Elimu. Inasemekana kwamba chema chajiuza na kibaya--- Sitaki kuumalizia msemo huu. Bw. Naibu Spika wa Muda, ombi langu la mwisho linahusu maslahi ya wakazi katika sehemu kame za nchi hii. Sehemu kame ya nchi hii si wilaya katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki peke yake. Sehemu kame ya nchi hii ni kubwa zaidi. Sehemu kame za humu nchini zinahitaji 2548 PARLIAMENTARY DEBATES July 17, 2007 kuzingatiwa kikamilifu, kwa sababu miaka 40 iliyopita, sehemu hizo zilidhulumiwa kupita upita uwezo wa mwanadamu yeyote. Kuziinua sehemu hizo, kimaendeleo, kwa muda wa miaka minne ni vigumu. Kwa hivyo, ninaiomba Wizara ianzishe sera itakayoshughulikia maslahi ya sehemu kame kwa njia maalum zaidi kuliko sehemu nyingine nchini. Kwa nini? Kwa sababu dhuluma ya miaka 40 ni dhulumu kubwa sana. Kwa hayo machache, ninaiunga Hoja hii mkono."
}