GET /api/v0.1/hansard/entries/213986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 213986,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213986/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wamwere",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
    "speaker": {
        "id": 352,
        "legal_name": "Koigi Wamwere",
        "slug": "koigi-wamwere"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi ili nichangia mjadala huu kuhusu Hoja hii ya bajeti ya Wizara ya Usalama wa Ndani. Bw. Spika, ningependa kuanza kwa kusema kwamba katika kupigana vita dhidi ya uhalifu, ni muhimu watu wetu wafundishwe kuheshimu polisi, kama marafiki na walinzi wao. Wanafaa kuacha kuwaona kama adui. Kwa hivyo, ni jambo la kuhuzunisha na makosa makubwa mtu anaposikia kwamba polisi wameshambuliwa na kuuawa wakiwa kazini. Kama wengi wa Wabunge wenzangu walioongea hapa jana, naamini pia kwamba polisi wanastahili bima. Bima hii itahakikisha kwamba kwa bahati mbaya askari akikutana na kifo, familia yake itashughulikiwa. Pia, polisi wanastahili mishahara mizuri na nyumba. Kwa mfano, ni makosa makubwa kumuweka mtu mmoja ambaye ana bibi kuishi katika chumba kimoja na mwingine ambaye hana bibi. Hiyo ni kuvuruga unyumba. Hili ni jambo ambalo limeendelea kwa muda mrefu. Inashangaza kwamba hata wakati huu ambao uchumi umekuwa, tumekosa pesa za kuwajengea polisi nyumba wanazostahili. Nadhani kuna kasoro kubwa katika jambo hilo. Natumahi kwamba Waziri ataona cha kufanya. Bw. Spika, pia, kuna shida ya kutegemea askari kufanya kazi na huku hawapewi magari wanayohitaji. Polisi hawawezi kufanya kazi bila magari. Ni lazima wasaidiwe na magari wanayohitaji. Bw. Spika, siwezi kusisitiza zaidi kwamba mishahara mibaya huzaa ufisadi. Ikiwa tunataka polisi waache kuwa wafisadi, basi ni lazima tuwaongezee mishahara. Pamoja ya hayo yote ambayo nimesema, ningetaka pia kuongeza kwamba polisi wanafaa kufundishwa kufanya kazi kitaaluma. Wanafaa kufundishwa sheria, kwa sababu wanafaa kufanya kazi yao kwa mujibu wa sheria. Ikiwa hawajui sheria hiyo, hawawezi kuitimiza wakiwa kazini. Lazima polisi wafundishwe kutofanya kazi kama zamani. Wengine wetu tulikiona kilicho mtoa kanga manyoya, mikononi mwa polisi. Ni maombi yangu kwamba yale mateso tuliopitia, hakuna ambaye atayapitia leo, baada ya kupata mabadiliko. Lakini hilo haliwezekani mpaka polisi wafundishwe kuachana na namna ya zamani ya kufanya kazi. Bw. Spika, kuna wakati ambapo nilisikia kwamba polisi walikuwa wanafundishwa au kupewa masomo ya haki za kibinadamu. Sijui kama masomo hayo bado yanaendelea au la. Hii ni kwa sababu mtu akisoma magazeti yetu, ni kama kwamba polisi wamesahau haki za kibinadamu. Wanawakata watu kwa sababu ni washukiwa. Ningependa kusema kwamba nchi yetu inatawaliwa na demokrasia na kwa mujibu wa sheria. Kwa hivyo, polisi katika mfumo wa demokrasia, wanafaa waelewe pahali pao. Chini ya demokrasia, polisi hawawezi kuwa kila kitu. Hawawezi kuwa Wabunge wa kuunda na kupangua sheria. Hawawezi kuwa wao ndio wanaotoa mashtaka na wakati huo huo wawe mahakimu na wanamagereza. \"Mhe. polisi\", kihalali---"
}