HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 213990,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/213990/?format=api",
"text_counter": 184,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Spika ni ofisa mkuu wa Bunge. Bw. Spika, kihalali, polisi ni mkono wa Serikali wa kutekeleza sheria, kwa mujibu wa sheria. Bunge nalo linaunda sheria. Mahakama hutafsiri sheria na kutoa hukumu na adhabu. Kwa mujibu wa mpangilio huu, hata kama ameshikwa mshukiwa wa uhalifu wowote, hana hatia mpaka ahukumiwe na mahakama, ili imuachilie au impe adhabu. Hii ni kanuni muhimu ambayo inafaa kufuatwa na polisi. Nasema hivi kwa sababu, kama kazi ingekuwa inafanywa vile inavyofanywa sasa--- Tungekuwa tunaendelea na utawala uliopita, nadhani wengine wetu hatungekuwa hapa tukiongea. Tungekatwa zamani kama wahalifu. Mara nyingi tulishikwa kama washukiwa, lakini kwa bahati nzuri, tulipelekwa vizuizini na kufungwa jela hata kwa mambo ambayo hatukuwa tumeyafanya. Lakini hatukupigwa risasi. Kama tungepigwa risasi hatungekuwa hapa. Bw. Spika, kwa sababu Kenya ni nchi ya kidemokrasia na inatawaliwa na sheria, kimsingi, polisi hawana haki ya kuwaua washukiwa. Kazi yao kubwa ni kuwashika na kuwapeleka mahakamani ili wahukumiwe na kupatiwa adhabu. Hata hivyo, ukiyasoma magazeti kila siku, utagundua kuwa washukiwa wanauawa kila siku. Kwa mfano, utasoma kuwa jana polisi waliwaua washukiwa nane, juzi wakawaua 12 na mtondo wakawaua 20. Mtu anayesoma magazeti kila siku atafikiria kwamba kuna vita humu nchini kama vile vilivyoko nchini Iraq. Wakati mwingine unashindwa kutofautisha hali hizi mbili kwa sababu kule nchini Iraq ni Wamarekani na Waarabu, lakini hapa kwetu ni Serikali na wahalifu. Lakini hata hivyo, hali ni ile ile kwamba nchi imo katika vita. Hali hii haiwezi kuitwa jina lingine. Hata mara kwa mara, tunasikia kwamba wanafunzi wameuawa kama washukiwa. Aidha, tumemsikia mhe. Waziri akilia kwamba huko kwake watu wamesumbuliwa na polisi. Mambo haya yote yanamlazimisha mtu kuuliza, \"Tufanye nini?\" Bw. Spika, nitarudia kwa kusema kwamba kazi kubwa ya polisi ni kushika wahalifu wala si kuwaua. Mshukiwa hana hatia na hastahili kuuawa mpaka atakapohukumiwa na mahakama. Kuua mshukiwa ikiwa hakuwashambulia polisi, ni kuvunja sheria. Polisi kuwatolea washukiwa adhabu nje ya mahakama ni kuvunja sheria. Adhabu ya kila uhalifu siyo kifo. Kama kila uhalifu utaadhibiwa na kifo, basi hakutakuwa na magereza tena. Polisi watakuwa ndio magereza, mahakama, Bunge na kila kitu. Bw. Spika, ningependa kuongeza kwamba bunduki ya polisi siyo mwarubaine wa kumaliza uhalifu. Kumaliza uhalifu kunahitaji mbinu zaidi. Mojawapo ya mbinu za kumaliza uhalifu ni kumaliza umaskini. Tumeambiwa kwamba hakuna uhusiano kati ya umaskini na uhalifu. Umaskini unazaa uhalifu na hata unazaa wendawazimu! Wahalifu wengi pamoja na watoto wao ni maskini. Unashindwa kuelewa, kama umaskini hauna uhusiano na uhalifu, kwa nini wahalifu wengi ni watu maskini au watoto wao? Tumeona watu wakipigania mashamba na maji. Haya ni matatizo ya watu maskini wala siyo ya matajiri. Wale ambao wanasema kwamba umaskini hauna uhusiano na uhalifu, ningependa waniambie ni kitu gani basi kinachowavutia watu maskini kufanya uhalifu? Ni kitu gani? Kuna wale watakaosema kwamba ni uovu wa kuzaliwa nao ambao dawa yake ni risasi ya polisi tu. Sikubaliani nao! Mimi naamini kwamba ili kumaliza umaskini, ni muhimu kuongea na jamii zinazozaa wahalifu kwa wingi. Wale wanaopinga mazungumzo, wakumbuke kwamba Bunge hili lilipoteza Wabunge watano wakati walipotumwa na Wizara hii kwenda huko Marsabit na Turbi kuongea na watu ambao walikuwa wanafanya uhalifu. Bw. Spika, tusipozingatia mazungumzo, tutakuwa tunawasaliti hawa waliokufa. Tunahitaji kongamano la kitaifa ili tuongee swala hili ikiwa tunataka kumaliza vita ambavyo vinaendelea wakati huu. Yeyote ambaye atasema kwamba polisi waruhusiwe kufanya kila watakalo, ajue kwamba anatangaza utawala wa polisi. Huo utawala wa polisi ni udikteta kwa jina lingine. Sisi tuliotoka kule, hakuna kitu kinachotutisha kama kusikia kwamba nchi inaweza kurudi nyuma ikawa na udikteta tena. Bw. Spika, mwisho, ningependa kuwauliza polisi wawasaidie wapiga firimbi. July 12, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 2491 Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}