HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 214790,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/214790/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kingi",
"speaker_title": "The Assistant Minister, Office of the President",
"speaker": {
"id": 248,
"legal_name": "Joseph Kahindi Kingi",
"slug": "joseph-kingi"
},
"content": " Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo inaendelea. Kwanza ningependa kusema kwamba naunga mkono Hoja hii. Ningependa pia kuwapongeza wenzangu ambao wameiunga mkono. Kama vile tusemavyo maji ni uhai, vile vile usalama ni maisha na maendeleo. Hakuna maendeleo ya maana ambayo yanaweza kufanyika katika mazingira ambayo hayana usalama. Usalama unahitajika katika shule, ukulima, uuguzi na kila mahali katika taifa letu. Usalama hupatikana mahali ambapo mifumo iliyowekwa na Serikali na wananchi inafanya kazi. Mahali ambapo mifumo hii haifanyi kazi, mambo mengi huharibika. Mambo mengi yakiharibika, mambo hayo huzaa utovu wa nidhamu na kufanya usalama kuwa haba. Tumeishi katika nchi hii na Bara letu la Afrika pia kwa miaka mingi, katika hali ambayo mifumo iliyowekwa haikufanya kazi. Kwa mfano, ikiwa ni mfumo wa ugawaji wa ardhi, sheria iliyowekwa haikufuatwa kwa miaka mingi. Vile vile, tumeishi katika hali ambayo mifumo iliyowekwa ili kugawana kazi katika taifa haikufanya kazi. Tumeishi katika hali ambayo mifumo iliyowekwa ili kuimarisha vyombo vya usalama, kama vile vinavyotumiwa na polisi, haikufanya kazi. Kwa sababu tumeishi katika hali hiyo kwa miaki mingi, imekuwa ni hali ya maisha. Watu sasa wamechukulia utovu wa nidhamu na uvunjaji wa sheria kama kwamba ndio hali ya maisha. Leo ningependa kusema kwamba tuliishi katika taifa hili kama vile watu huishi katika kilabu cha usiku, ambako kila jambo huendelea. Leo tumekuja na nia ya kukisafisha kilabu hicho cha usiku na kukifanya mahali pa kuabudu; mahali pa utakatifu. Hio sio kazi rahisi, bali ni vita. Watu wameishi kwa kukuza na kuiuza bangi na kutengeneza pesa kinyume na sheria. Serikali imetangaza vita dhidi ya visa kama hivyo. Kwa hivyo, jamii zote ambazo zilikuwa zinategemea bangi kwa maisha, sasa zina vita na Serikali. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa muda mwingi tuliishi katika hali ambapo vijana wengi walitengeneza pesa katika biashara ya matatu bila kufanya chochote. Leo hii tunawaambia hatutaki hali hiyo iendelee. Tukifanya hivyo, inakuwa ni vita. Watu wamekuwa wakileta bunduki hapa nchini na kuziuza ili watengeneza pesa. Leo tunasema jambo hili ni haramu. Mtu aliyepata ardhi kinyume cha sheria lazima arejeshe ardhi hiyo kwa Serikali na ipewe wananchi wengine kulingana na sheria. Jambo hili pia haliwezekani kwa sababu ni vigumu kufanya hivyo. Ikiwa nafasi za kazi zilienda kwa sehemu moja ya taifa, sasa tunataka kila mtu apate. Hata hivyo, itatubidi labda tupunguze hapa ili tuongeze pale. Jamo hili haliwezekani. Mambo kama hayo yanaweza kuleta vita hapa nchini. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninataka kusema kwamba leo tunataka kubadilisha mambo. Tukifanya hivyo, basi tutapata pingamizi kila mahali. Kwa hivyo, hali inayoendelea leo, tulikuwa tunaitarajia wakati ule tunataka tufanye marekebisho ya maisha yetu. Kupiga vita hivi si rahisi kwa sababu gharama yake itakuwa juu. Ni lazima taifa likubali kutumia pesa na raslimali ili tuweze 2462 PARLIAMENTARY DEBATES July 11, 2007 kushinda vita hivi. Ndio maana ninamuunga mkono Waziri anaposema ya kwamba hata pesa ambazo Wizara yetu imetengewa katika bajeti ya mwaka huu, hazitoshi. Pesa hizi ni nusu ya mahitaji yetu. Tunahitaji zaidi ili tuweze kuhakikisha ya kwamba mifumo ile ambayo iliwekwa inaweza kufanya kazi. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninazungumza juu ya askari wetu ambao wana jukumu kubwa la kulinda usalama na mali ya wananchi. Idadi yao ni chache muno. Hawatoshi. Ni lazima tuhakikishe ya kwamba tunawaongeza marudufu. Tunajua mishahara yao ni ya chini sana. Huwezi kumlipa Kshs5,000 mtu ambaye kazi yake ni kulinda usalama na maisha ya watu ambao wana mabilioni ya pesa. Kwa hivyo, ni lazima katika bajeti yetu tuwafikirie. Si mishahara yao tu, bali tuimarishe makazi yao. Askari wetu wengi wanaishi vibandani ambavyo vinavuja. Ni vyumba ambayo havifiki futi kumi kwa kumi na huko anatarijiwa kwenda kumlinda mtu ambaye nyumba yake ni vyumba zaidi za 20. Ni mtu ambaye analala vizuri na ana mali nyingi. Ninasema ni lazima turekebisha mahali wanapokaa. Marekebisho haya yanahitaji pesa. Vyombo vyao vya kufanyia kazi ni lazima viimarishwe. Vinunuliwe vya kisasa. Tusiwanunulie vyombo hivi tu, ni lazima viifadhiwe. Ni jambo la kuchekesha kuona ya kwamba wilaya nzima wakati mwingine inapewa Kshs50,000 au hata Kshs100,000 ya kuhifadhi, kulinda na kurekebisha vifaa vya kufanyia kazi. Ikiwa magari yatafanya kazi kwa siku mbili kwa mwezi na muda ule mwingine wote hayafanyi kazi, hatuwezi kuendelea. Tunahitaji pesa kwa kuhakisha ya kwamba askari wetu wana vifaa vya kutosha. Wale waliosema ya kwamba kila mkoa unahitaji kuwa na helikopta ili tuhakikishe usalama umeimarika na panapotokea matatizo maofisa wetu wanafika kwa haraka. Labda jambo hili lingekuwa limetekelezwa miaka mingi iliyopita. Sasa sisi tumechelewa kufanya kwa hivyo tutahitaji kutumia pesa nyingi kwa wakati mmoja ili kuhakisha ya kwamba vifaa kama hivyo vinapatikana ndio tuweze kuendelea kufanya kazi yetu vizuri. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumezungumza kuhusu askari wale ambao wanapoteza maisha wakati wa kazi. Ni muhimu kufikiria jamii zao. Watoto watafutiwe shule ambapo wataendelea na elimu yao bila kutatizwa. Afya yao ihakikishwe ya kwamba inatunza na waweze kupata matibabu bila malipo. Pia waweze kupata chakula ili maisha yao yaweze kuendelea bila shida. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumeanzisha wilaya nyingi kwa sababu tunataka kuhakikisha ya kwamba huduma kwa mwananchi iwe karibu na yeye haraka iwezekanavyo. Hatutaki wakati ule wa zamani ambapo mtu anatumia siku mbili au saa kumi akisafiri kutafuta mkuu wao wa wilaya. Hizi wilaya mpya ambazo tumezindua na hata zile za zamani zinahitaji vifaa ili kuweza kutoa huduma. Tunahitaji kumpatia mkuu wa wilaya ofisi safi, nzuri na kubwa na pia vifaa vya kisasa kutumikia wananchi. Tunahitaji kuwapatia wakuu wa tarafa na lokesheni vifaa vya kisasa ili waweze kuwatumikia wananchi. Bw. Naibu Spika wa Muda, tunazungumza habari ya kununua pikipiki kwa machifu wetu. Labda tunafanya hivyo kwa sababu ya hali yetu ya umasikini au udhaifu. Ninasema hata pikipiki hazifai kwa watumishi wa umma kama machifu. Tungekuwa tunazungumzia juu ya magari ambayo wanaweza kuyatumia. Pengine tungewanunulia pikipiki manaibu wao. Bw. Naibu Spika wa Muda, miaka mingi hatukuweka rasilimali yetu katika usalama wetu. Sasa hali imekuwa mbaya. Ni lazima tukubali ya kwamba ilituweze kurekebisha hali ya usalama wetu, ni lazima tutumie raslimali yetu. Kwa hivyo, Waziri anaposema kwamba tutarudi hapa hivi karibuni kuuliza Bunge kutuongezea pesa katika bajeti yetu ili tuweze kufanya mambo haya yote ambayo Wabunge na wananchi wanataka sisi tuyafanye; nina amini anasema jambo ambalo ni la kweli na litaungwa mkono na Wabunge wakati utakapofika. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}