GET /api/v0.1/hansard/entries/215134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 215134,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/215134/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, pasipoti ya Kenya ni lazima iheshimiwe na ichukuliwe kwa uzito unaofaa bila kujali ni mtu gani ambaye anaibeba. Wasomali ni Wakenya. Ikiwa Msomali wa Kenya ambaye ana pasipoti ya Kenya akienda Tanzania anakamatwa na Serikali 2304 PARLIAMENTARY DEBATES July 5, 2007 haiwezi kumlinda, lazima Serikali ichukue msimamo. Je, Waziri anachukua hatua gani ili kuhakikisha kwamba Jamhuri ya Tanzania inahesimu pasipoti ya Kenya, iwe imebebwa na Msomali au mtu gani? Hatutaki watu wetu wabaguliwe na hali hatuwabagui Watanzania ambao wako katika nchi yetu."
}